Your Basket

Checkout | Shopping Cart
Jenga Nidhamu Kali - GetValue
Biashara & Ujasilimia Mali

JENGA NIDHAMU KALI

0.2
1
  • 5
  • 4
  • 3
  • 2
  • 1
Price:
10,000 Tsh.
Vendor:
Added To Cart:
0
Added to shop:
Jul 10, 2023
Product Views:
251
In category:
Sample

Amsha Nguvu Ya Kujisukuma Ili Kutimiza Malengo Yako

Kamarnmafanikio yangekuwa ni mipango pekee basi kila mtu angekuwa nayo maradufu. Kilarnkitu ambacho mtu anakitamani akipate maishani mwake kingekuwa tayari kipornmikononi mwake. Kumekuwa na matamanio na mipango mbalimbali ya kupata mafanikiornlakini kwa bahati mbaya watu wengi hawana mafaniko hayo.

 

Kama ukisema ukusanye malengo ambayo watu wanayo,rnutagundua kuwa watu wana malengo na mipango mizuri lakini ni mipango michachernsana inayozaa matunda.  Hapa kutakuwa narnshida sehemu. Kwa nini watu wanajua nini cha kufanya lakini hawana matokeo?

 

Mwakarnmpya ukifika kila mtu huwa na hamasa kubwa ya kufanya makubwa. Huu huwa ni mudarnwa shauku kubwa na shamra shamra huku kauli ile ya mwaka mpya na mambo mapyarnikitoka midomoni mwa watu wengi. Mwaka huu lazima nifanye makubwa. Mwaka huurnlazima niongeze kipato changu. Mwaka huu lazima nikuze biashara yangu. Mwakarnhuu lazima nisome vitabu vingi sana, mwaka huu lazima niandikie kitabu nk..

 

Wapo ambao huandika kabisa malengo hayo lakini wapornambao huyafikiri tu vichwani mwao. Hamasa hizo huwafanya watu wengine watangazernnini wanachotarajia kukifanya.

 

Lakini baada ya muda mfupi kama miezi miwili hamasarnhiyo huanza kuisha na kutowasikia wakitaja tena nini wanataka kukifanya. Baadarnya shamra shamra hizo kuzima, watu hurudi kuishi maisha yao ya kawaida ya mwakarnjana ambayo hayakuwa na mafanikio. Kuna shida kubwa ambayo inatenganisha mipangornna mafanikio, shida hiyo ni NIDHAMU KALI.

 

Nidhamu ni kiungo kinachosimama kati ya malengo narnmatokeo. Nidhamu ndiyo inayowezesha kazi inayotakiwa mtu aifanye ile apaternmatokeo. Nidhamu kali ni kufanya kile ulichopanga kukifanya bila kuruhusurnsababu yoyote ikuzuie. Malengo peke yake hayatoshi yanahitaji kazi ili kutoarnmatokeo. Mtu anapotaka kuweka kazi ili kupata matokeo, ndipo vikwazo vingirnhuanza kujitokeza. Vikwazo hivyo mara nyingi huambatana na maumivu.

 

Ili kuweza kuchukua hatua za kupata matokeo licha yarnchangamoto hizo unahitaji msukumo usio na ukomo, hii inaitwa nidhamurnkali. Nidhamu ni kumbishia mwingine anayesema usifanye kile ulichopangarnkufanya.  Kwamfano umepanga kuanza kuamkarnmapema ili kuianza siku mapema na kwa mafanikio, muda wa kuamka ukifika, kunarnmwingine anasema uendelee kulala na kwa nini ujitese! Nidhamu kali ni kumbishiarnhuyu na kumshinda.

 

Kumshinda mwingine anayekubishia ni ushindi juu yarnmtazamo wako. Vikwazo vyote unavyokutana navyo vinaanzia kwenye akili yako,rnyaani unavyochukulia jambo. Kabla ya kuomba mwili wako umshinde mwingine na hunarnbudi kuushinda mtazamo unaoshindana na wewe.

 

Nidhamu narnmafanikio: Nidhamu na mafanikio nirnmapacha. Watu wamejaribu kuwatenganisha mapacha hawa lakini imeshindikana.  Hii ni kwasababu hakuna mafanikio yoyote bilarnkuweka kazi. Lakini kufanya kazi sio zoezi rahisi kwasababu ya ugumu unaowezarnkukutana nao. Nidhamu pekee ndiyo itakusaidia ujisukume uchukue hatua na kupatarnmafanikio.

 

Kujengarnnidhamu. Nidhamu ni kiturnkinachojengwa. Kuna hatua za kupitia na inahitaji muda pia ili kuwa na nidhamurnyenye msimamo.  Kujenga nidhamu kali yarnkukuwezesha kufanya jambo lolote bila kujali maumivu au vikwazo vyovyote, sirnkazi rahisi ndiyo maana watu wengi hawafanikiwi. Kiungo kikuu cha kujengarnnidhamu ni kujua KWA NINI KUBWA yarnkufanya kitu hicho. Hii ni sababu ambayo itashinda  nguvu ile ya kukuzuia kufanya jambo hilo.rnHiki ni kitu utakachokipata kwa kujisukuma kuchukua hatua.  Je ni kupata uhuru wa kifedha? Je ni kuwa narnafya njema ya kudumu? Utafanikiwa kujenga nidhamu kali kama utafanikiwarnkuifahamu kwa nini yako kubwa.

 

Nidhamurnbinafsi. Kuna aina nyingi za nidhamu ambazornmwanadamu anaweza kuzijenga lakini binafsi ndiyo nidhamu mama. Huu ni ushindirnjuu ya ukinzani mkubwa wa kutochukua hatua unaokutana nao ndani yakornmwenyewe.  Ukishaweka malengo kisharnkuanza kuweka kazi, ukinzani utaanzia ndani yako mwenyewe. Unahitaji kijikanarnnafsi yako kuwa kuna chaguo moja tu kwenye kile ulichopanga kufanya, nacho nirnmatokeo na sio sababu. Katika kufanikiwa kuijenga nidhamu binafsi UVUMILIVU nirnkiungo muhimu sana.

 

Nidhamu yarnmuda. Muda ni mali. Muda ni fedha.rnHii ni misemo inayoashiria ni kwa namna gani muda ulivyo muhimu sana kwenyernmafanikio. Utafanya chochote kama utakuwa na muda. Lakini pia mafanikio mengirnyanachukua muda mrefu kutokea hivyo kadri utakavyokuwa unapoteza muda ndivyornutakavyochelewa kupata mafanikio au hata kuyakosa kabisa. Kufanikiwa ni kutumiarnmuda kwa ufanisi mkubwa. Hii inawezekana na kujenga nidhamu kali ya muda.rnHuwezi kutunza muda bali kuutumia vizuri.

 

Nidhamu yarnfedha. Fedha ni neno lililokaa sanarnakilini mwa watu wengi. Jitihada nyingi zinazofanywa na binadamu zinalengarnkupata fedha. Hii ni kwasababu fedha inatatua changamoto nyingi. Utakuwa narnuhuru mkubwa kama utakuwa na fedha za kutosha. Licha ya watu kuwa na uhitajirnmkubwa wa fedha, lakini imekuwa siyo rahisi kuwa na fedha nyingi za kukuparnuhuru. Unahitaji msukumo mkubwa wa kuchukua hatua ulizoziweka kwa ajili ya kuzalisha,  kuweka na kuthibiti fedha.  Hii ni nidhamu muhimu unayotakiwa kuijenga.

 

Nidhamu yarnkazi. Kuna rafiki mmoja ambayernukiambatana naye kwenye safari ya kuyafikia mafanikio hatakuacha kamwe. Nirnmwaminifu sana. Bahati mbaya ni rafiki ambaye huwezi kumwepuka kama kwelirnunataka matokeo. Rafiki huyu ni kazi. Hakuna mbadala wa kazi. Hakuna matokeornyoyote bila kazi.

 

Pia kazi hutangulia mafanikio, hujaweka kazirnusitegemee mafanikio yoyote. Watu wengi wamekuwa wakikwepa kazi huku wakiaminirnkuwa watafanikiwa bila kazi. Mwili wako kwa asili ni mvivu. Unahitaji msukumornmkubwa kutoka ndani yako ili kuweza kuweka kazi katika mipango yako kisharnkupata matokeo. Hapa ndipo kitabu hiki kitakapokusaidia wewe kujenga nidhamurnkali ya kazi ili uweze kupata mafanikio.

 

Toa matokeornsiyo sababu. Kwa sababu kazi ndiyorninayotoa matokeo na watu hawapendi kuweka kazi kwa sababu ya maumivu, hivyornhutafuta sehemu ya kukimbilia. Kimbilio pekee huwa ni kutoa sababu kwa ninirnhawawezi kufanya kazi. Hiki ndicho kilichowaponza watu wengi walioshindwa.

 

Wana utajiri wa sababu za kwa nini wameshindwarnkuchukua hatua badala ya utajiri wa matokeo ya kuwapa mafanikio.  Utafanya nini ili utoe matokeo na sio sababu?rnKitabu hiki kitakupa mwongozo wa kujenga nidhamu itakayokusaidi kujisukumarnkuchukua hatua kisha kupata matokeo badala ya kukimbilia kutoa sababu.

 

Ili nidhamu iwe msaada katika maisha yako, inapaswarnlisiwe tukio bali sehemu ya maisha yako. Hivyo ili kufanikiwa kujenga nidhamurnya kudumu huna budi kuifanya kuwa tabia yako. Utafanikiwa hilo kama utaifanyarnkuwa sehemu ya maisha yako. Kwamfano ili kuwa na afya njema, weka kufanyarnmazeozi kila siku kama sehemu ya maisha yako. Kitabu hiki kitakusaidia namna yarnkuifanya nidhamu kuwa tabia.

 

Ndugu ndoto zako zitatimia, kusudi lako utaliishi kikamilifurnna utatimiza malengo yako kama utafanikiwa kujenga tabia hii muhimu ya nidhamurnmaishani mwako.  Hii ndiyo itakayokusaidiarnkuamsha nguvu kubwa iliyolala ndani yako ya kufanya mambo makubwa. Kitabu hikirnni mwongozo sahihi wa kukusaidia kujenga nidhamu kali muhimu katika maisha yako.rnKisome na chukua hatua zilizopendekezwa kwenye kila mwisho wa sura. Hakikarnmafanikio yatakuwa upande wako.

 

Nakutakia kila la kheri. 

rnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrnrn

Alfred Mwanyika 

More Products On Discount
7,000 Tsh. 2,999 Tsh.

Sold by: Said Maumba

10,000 Tsh. 9,000 Tsh.

Sold by: Godius Rweyongeza

10,000 Tsh. 7,000 Tsh.

Sold by: Godius Rweyongeza

2,000 Tsh. 1,000 Tsh.
(5.4)

Sold by: Gaston Ngailo

3,999 Tsh. 1,999 Tsh.

Sold by: Daudi Lubeleje

6,000 Tsh. 5,000 Tsh.

Sold by: Godius Rweyongeza

Best Sellers List
Best Seller
2,000 Tsh.
(5.4)

Sold by: Gaston Ngailo

Best Seller
10,000 Tsh.
(69.8)

Sold by: Samuel Macha

Best Seller
3,000 Tsh.
(16.4)

Sold by: ABDULKADIR MASSA

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PETER TARIMO

Best Seller
4,000 Tsh.

Sold by: Mashaka Khamis

GetValue Recommendations
5,000 Tsh.

Sold by: Denis Mpagaze

10,000 Tsh.
(1)

Sold by: PJ PROJECTS

12,000 Tsh.

Sold by: Germano Mbelwa

5,000 Tsh.

Sold by: Sabas Patrick

25,000 Tsh.

Sold by: PJ PROJECTS

Old is Gold