Your Basket

Checkout | Shopping Cart
Maisha Ya Masikini Mwelevu - GetValue
Biashara & Ujasilimia Mali

Maisha Ya Masikini Mwelevu

0
0
  • 5
  • 4
  • 3
  • 2
  • 1
Price:
10,000 Tsh.
Vendor:
Added To Cart:
0
Added to shop:
Jan 23, 2026
Product Views:
87
In category:
Sample

Masikini Mwelevu aoni ugumu wa maisha kama kikwazo kwake kuyafikia mafanikio

       “Kila kizazi kina walalamikaji wake, lakini wachache sana wanaochagua kusimama na kubadilisha hadithi zao.” (Sehewa Edward Mohamed 2025)


Kitabu hiki ni zao la safari, si mawazo ya ghafla. Ni matokeo ya miaka ya tafakari, maumivu, maombi, na mapambano ya maisha ambayo yamenifundisha jambo moja kuu kwamba kuna tofauti kati ya masikini wa mali na maskini wa akili.


Nilianza safari hii nikiwa na swali moja tu: Kwa nini watu wengi tuna ndoto nzuri, lakini wachache sana huzitimiza?

Kadri nilivyozidi kuangalia maisha ya watu waliofanikiwa na wale waliokata tamaa, niligundua kitu cha ajabu — tofauti haiko kwenye bahati, elimu, wala nasaba; tofauti ipo katika mtazamo na uamuzi wa mtu kuamini kwamba anaweza kubadilika.


Dibaji hii ni kioo cha moyo wangu kwa msomaji. Ninakualika usisome kitabu hiki kama hadithi ya kufurahisha, bali kama safari ya kujitambua. Kila ukurasa umebeba chembe ya ukweli, kila simulizi limepakwa jasho la uzoefu, na kila fundisho limevutwa kutoka kwenye maisha halisi ya mapambano ya kila siku.



Nilipoanza kuandika “Maisha ya Masikini Mwelevu”, sikuwa na lengo la kuandika kitabu kingine cha “motisha” tu bali nilitaka kuandika mwanga wa matumaini — mwanga utakaopenya katika giza la hofu na kukata tamaa lililomea kwenye mioyo ya watu wengi.

Nilitaka kuandika maneno yatakayomfanya kijana asiye na kazi aamini tena katika ndoto yake; mzazi anayelia na majukumu aone sababu ya kuendelea kupigana; na mtu aliyeshindwa mara nyingi aamini kwamba kushindwa si mwisho — ni mwanzo wa uelewa mpya.


Kitabu hiki kimejengwa juu ya misingi  mikuu mitatu:


1. IMANI: Kwa Mungu, kwa ndoto zako, na kwa uwezo uliopewa ndani yako.


2. NIDHAMU: Uwezo wa kufanya maamuzi sahihi hata pale moyo unapokataa.


3. UVUMILIVU: Uwezo wa kungoja wakati wa Mungu bila kukata tamaa.


Katika kila sura utakutana na simulizi zinazogusa uhalisia wa maisha, mafunzo ya hekima, na maswali ya tafakari yatakayokusaidia kufikiri kwa kina kuhusu maisha yako na mwelekeo wako. Utakutana na sauti ya kipekee inayosema: “Wewe si mdogo kama unavyofikiri.”


Naamini kuwa “masikini mwelevu” ni yule anayejua hali yake ya sasa, lakini hataki ibaki hivyo. Ni mtu anayeamka kila siku akiwa na imani kwamba Mungu ana mpango mpya wa maisha yake. Ni mtu anayepanda mbegu leo kwa machozi, lakini kesho atavuna kwa furaha.

Dibaji hii ni shuhuda kwamba nilichoandika si ndoto tu bali ni uhalisia.

Ni ushuhuda wa kwamba Mungu anaweza kumuinua mtu yeyote, mradi tu moyo wake umejawa na imani, uvumilivu, na uamuzi wa kubadilika.

Ni sauti ya wito kwa kizazi hiki: Tuanze kufikiri kama washindi, tuishi kama watu wa kusudi, na tuamke kama watenda kazi wa Mungu.


“Usiogope kuanza ukiwa peke yako, kwa sababu hata mwanga huanza kwa cheche moja.”


Nakualika sasa, msomaji wangu, ufunge mikanda ya safari hii. Tunaingia kwenye dunia ya uhalisia, imani, na hekima. Safari ya “Masikini Mwelevu” si hadithi ya mbali bali ni hadithi yako, hadithi yangu, na hadithi ya kila mtu anayeamini bado ana nafasi ya kushinda.


More Products On Discount
Best Sellers List
Best Seller
1,000 Tsh.
(5.4)

Sold by: Gaston Ngailo

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PASTOR TONY OSBORN

Best Seller
10,000 Tsh.
(69.8)

Sold by: Samuel Macha

Best Seller
3,000 Tsh.
(16.4)

Sold by: ABDULKADIR MASSA

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PETER TARIMO

Best Seller
150,000 Tsh.
(3.6)

Sold by: Gaston Ngailo

GetValue Recommendations
Old is Gold