
NATAMANI KUANZA KUSOMA VITABU
Mwongozo Wa Kujenga Tabia Ya Kusoma Vitabu. Katika kitabu hiki utapata kujifunza mambo yafuatayo; 1. Faida za kusoma Vitabu 2. Kwanini watu hawasomi vitabu 3. Namna ya Kujenga Tabia ya Kusoma Vitabu. 4. Kanuni ya 2 × 3 × Akili: Ukiifahamu kanuni hii hautawahi kuishiwa pesa mfukoni. 5. Tovuti zaidi ya 20 za kupata vitabu bure mtandaoni. 6. Orodha ya vitabu zaidi ya 100 unavyoweza kuanza navyo kuvisoma. 7. Namna ya kumjengea mtoto mdogo tabia ya kusoma vitabu. 8. Siri walizozificha matajiri kuhusu vitabu. 9. Siri walizoficha wanawake wanaosoma vitabu.
Pamoja na kuwa mwandishi wa vitabu 6 sasa na hiki kikiwa cha 7 mimi pia
ni msomaji mzuri wa vitabu na makala. Nimefanya kujifunza kama sehemu ya
maisha yangu na mojawapo ya kitu ninachofurahia. Mpaka sasa nimesoma
vitabu vingi sana na matokeo chanya ya usomaji wa vitabu nimeyaona.
Sijawahi kujutia kupoteza hata shilingi moja kwenye kununua kitabu
chochote kila kitabu nilichosoma kwa namna moja ama nyingine
kimenisogeza katika hatua fulani ya kimaisha. Naweza kusema kwangu mimi
dunia isiyo na vitabu ni sawa na kwamba umeninyima oksijeni. Bila
vitabu siishi.