Siri Ya Familia
Siri Ya Familia
Familia katika muktadha wa jamii ni muunganiko baina ya Baba, Mama na watoto ambao wanaishi pamoja kwa kushirikiana katika mambo mbalimbali yanayowahusu wao. Pia familia inajumuisha, Bibi, Babu na ndugu wengine wa karibu. Ndoa ni muunganiko wa hiari baina ya watu wawili wa jinsia tofauti waliopendana na kukubaliana kuishi pamoja kama mume na mke. Soma Mwanzo 2:21-24 Ndoa ni kitu kizuri sana katika maisha ya binadamu aliyekamilika kihisia. Isipokuwa kwa wale walio amua kuishi maisha ya kumtumikia Mungu pasipo kuoa au kuolewa mfano mapadri, masista, maburuda n.k. Familia ni kitu kinacholeta furaha katika maisha ya binadamu, na kinachoimarisha afya ya mtu pale familia au wanandoa wanapoishi kwa maelewano na masikilizano. Katika maisha ili ndoa na familia iweze kuwa imara watu hupaswa kuzingatia mambo kadha wa kadha. Kutokana na wosia mwingi unaotolewa wakati wanapofunga ndoa ukiwataka wapendane na kuvumiliana. Wosia huo ni wa ukweli kabisa, lakini je! Msingi wa yote haya watu hupaswa kufanya nini? Kushika mambo yanayoimarisha familia au ndoa.