AKILI YA PESA
Unapata pesa lakini zinaisha bila wewe kujua zimeishaje rnUnatamani kuweka akiba lakini haujui uanzie wapi na uweke wapi akiba yako ili izae rnUnatamani kuanza uwekezaji lakini haujui unaanzajernUnapata pesa nyingi lakini matumizi yanakuzidi kiasi kwamba unatumia pesa zako zote hubakishi hata kidogo. rnUmechoshwa na wimbi la madeni yanayokuandama kila mwezi na haujui utatoka vipi. rnrnKama wewe ni mmoja wa watu wanaopata hizi changamoto za kifedha basi kitabu hiki ndicho suluhisho lako kamili. rnrnAKILI YA PESA kinakupa mwongozo wa kujenga ufahamu wa kifedha utakaokusaidia kudhibiti na kutawala pesa zako na hatimaye kufikia uhuru wa kifedha. rnrnKumbuka, "fedha bila ufahamu wa kifedha, ni fedha itakayopotea ndani ya muda mfupi."
Mafanikio ya kifedha hayatokani tu na wewe kupata pesa nyingi bali ni matokeo ya wewe kuwa na nidhamu ya pesa unazopata hata kama ni kidogo. Na nidhamu ya fedha hujengwa na kiwango chako cha ufahamu wa kifedha.
Ukweli ni kwamba watu hawafanikiwi kifedha kwa sababu hawana pesa nyingi ila ni kwa sababu hawana ufahamu wa kifedha (akili ya pesa) ambao ndio msingi sahihi wa mafanikio ya kifedha.
Ndio maana kuna watu wamewahi kushinda pesa nyingi kwenye michezo ya bahati nasibu lakini baada ya muda wakarudi kwenye hali zao za kawaida. Hii inadhihirisha kwamba kuwa na pesa nyingi pekee hakutoshi kukufanya kufanikiwa kifedha bali kiwango chako cha ufahamu wa kifedha ambacho ndicho kinakujengea nidhamu ya pesa.
Mafanikio yako ya kifedha yanategemea jinsi unavyoitumia pesa inayopita mikononi mwako pasipo kujali kama ni kidogo ama ni nyingi.
Na namna unavyoitumia pesa inayopita mikononi mwako inategemea na ufahamu wako wa kifedha (akili ya pesa).
Sasa, yamkini umekuwa ukipata pesa nyingi lakini kila mara umekuwa ukijiuliza ni wapi pesa zako zinapokwenda kwani zimekuwa zikiisha kwa haraka huku ukiwa haujafanya kitu chochote cha maana.
Wakati mwingine suala la kupata pesa kwako limekuwa ni changamoto kiasi kwamba umekuwa ukijiuliza ni kitu gani ufanye ili uweze kupata pesa na kufanikiwa kifedha kama watu wengine, basi kitabu hiki ni kwa ajili yako.
Kupitia kitabu hiki utaenda kujifunza mambo muhimu ya kukusaidia kujenga ufahamu wa kifedha yaani akili ya pesa ambayo ndio msingi mkuu wa mafanikio ya kifedha. Haya ni mambo ambayo yamewafanya watu mbalimbali wakiwemo matajiri wakubwa duniani kufanikiwa kwenye eneo la fedha.
Mpaka kufikia mwisho wa kitabu hiki utakuwa umeweza kujenga ufahamu wa kifedha utakaokusaidia kufahamu namna ya kutengeneza
fedha, namna ya kutumia fedha, namna ya kuzalisha fedha na namna ya kuwekeza fedha
Sina shaka kuwa kupitia kitabu hiki utaenda kuanza ukurasa mpya wa maisha kwenye eneo la fedha na kuwa miongoni mwa watu watakaofanikiwa kifedha.
Kumbuka; \"kila pesa inayopita mikononi mwako ni mbegu ya kukuzalishia pesa zaidi kama utafahamu namna bora ya kuitumia.\"