KIPAJI CHAKO NI HELA
Kipaji chako ni zawadi toka kwa Mungu kuja kwako. MATUMIZI YA HICHO KIPAJI ni zawadi yako kwa Mungu. Wewe ndio muamuzi, lakini kuna maelfu ya watu duniani wamefanikiwa kujiajiri, kuzalisha bidhaa na huduma, na wengine wamefanikiwa kufungua makampuni. Yote ni baada ya kugundua vipaji vyao, kuviendeleza na kuvigeuza pesa.
Fikiria majina ya watu kama Mh Erick Shigongo, Diamond Platnumz, Mbwana Samatta na Mwakinyo.
Kitu gani kimoja wote wako nacho? KIPAJI.
Mh Shigongo amefanikiwa kutoka kwenye kuwa muandishi wa vitabu, mkufunzi, mfanyabiashara na hadi kuwa kiongozi.
Mbwana Samatta ni stori inayosisimua masikio ya vijana wengi wanaopenda soka. Kupitia yeye wazazi wengi wameruhusu watoto wao kucheza mpira, na kuuchulia mpira kama ajira ramsi kabisa.
Diamond Platnumz ndio haihitaji maelezo mengi kabisa, yote unayoyafahamu yanatosha kujieleza. Shule haikuwa sehemu yake kabisa, lakini kipaji chake kimefanikiwa kutengeneza dunia kwa wengi.
Mwakinyo, bado stori yake haijawa kubwa sana. Lakini itoshe kusema mikono yake ndio inampa kula, kupanda ndege na kufanya maisha.
VIPI KUHUSU WEWE?
Umekatia tamaa kuchora?
Umekatia tamaa uandishi?
Umeacha kabisa kuimba?
Hutaki tena kuigiza?
Hujiona kama wewe ni genius?
Kitabu hiki ni HABARI NJEMA KWAO. Ukiachana na kukupatia mkakati wa hatua kwa hatua namna ya kugeuza kipaji chako kuwa hela. Pia kimezungumzia kuhusu utafiti uliofanywa na Dr Howard Gardner, The Frames of Minds - Theory of Multiple Intelligence. Utafiti unaothibitisha kisayansi kabisa KILA MMOJA WETU ANA KIPAJI MAHALI FULANI!
Zawadi yangu, ninayompatia Mungu wangu kwa kunipa uwezo mkubwa wa kufikiri, kuumba maneno na kuandika. Ni kutoa vitabu vingi kadri inavyowezekana. WEWE UNAFANYA NINI???