FIKIRIA MARA MBILI
Fikiria mara mbili ni kitabu kinachofundisha kutokuchukua maamuzi bila kuchunguza
Chwi! Chwi! Chwichwi! Chwi! Sauti ya ndege aliyekuwa akilia juu ya nyumba yangu ndiyo iliyonitoa usingizini. Nilipofumbua macho, miali ya jua lililokuwa linachomoza ilikuwa inaingia taratibu ndani ya chumba changu kupitia dirisha la upande huu wa mashariki mwa nyumba.
Niliduwaa kama sekunde kadhaa nikipepesa macho kama vile ni mgeni ambaye ndiyo mara ya kwanza kuwamo chumbani humu.
Miali ya jua hili la asubuhi ilikuwa inaendelea kukipamba chumba changu hiki kidogo kwa rangi zake mbalimbali na kukifanya kionekane kizuri ajabu. Niliendelea kuwa pale kitandani nikistaajabia uzuri wa rangi za miali ya jua huku ndege aliyekuwako nje juu ya paa alikuwa anaanza kunikera sasa.
Ndege alilia kama ametumwa kuja kunitaarifu habari za majambazi wanaokuja kunivamia nyumbani kwangu naye ananionea huruma, na hivyo anajitahidi nimwelewe haraka. Saa ya ukutani nayo ilitoa mlio kuashiria kuwa saa moja asubuhi imetimia, hivyo natakiwa kufanya haraka kwani nimebakiwa na dakika kama ishirini tu za kukaa nyumbani vinginevyo nitakuwa ninaanza kuchelewa kibaruani.
Niliamka na kujivuta taratibu kulifuata taulo langu toka pale nilipolitundika jana yake, nikachukua na mswaki na kuelekea bafuni. Bila kuchelewa nilianza kuyateleza maji mwilini na sasa nilianza kufanya haraka.
“Hodi! Hodi!” Sauti ya kijana wa kiume ilisikika ikibisha hodi hapa hapa nyumbani kwangu. “Karibu!” nililazimika kuitikia japo nilikuwa bafuni kwani hakukuwa na mtu mwingine zaidi yangu. “Shikamo mwalimu” kijana aliniamkia. “Marahaba, nani wewe?” niliitikia na kuuliza swali. “Ni mimi Prisbert”, kijana alijibu
“Ahaa! Una shida gani?” nilimuuliza tena sababu sina kawaida ya kufuatwa na wanafunzi nyumbani kwangu hasa kwa nyakati kama hizi. “Kuna mzigo wako nimepewa na mama mmoja hapo stendi nikuletee,” kijana alieleza kwa ufasaha huku sauti yake ikionesha naye anafanya haraka kuwahi shuleni. “Basi niwekee hapo barazani nitaukuta” nilimwomba kijana huyo na na baada ya kufanya hivyo aliniaga na kuanza kuondoka kwa mbio.
Inaendelea....
PATA NAKALA YAKO SASA
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza