FUNGUO ZA UFALME WA MBINGUNI
Kila mlango unahitaji Funguo kuingia na kujionea thamani ya vilivyopo ndani yake, kadhalika Ufalme wa Mungu umesheheni siri na hazina tele ambazo pasipo kujua Funguo na namna ya kuzitumia ipasavyo katika maisha yetu katika Kristo itafanya tuendelee kuwe watumwa ikiwa sisi ni Wana wa Mungu. Hichi kitabu kinashusha Funguo mbalimbali katika Ufalme wa Mungu ni jukumu letu kujihusisha kikamilifu ili kuleta mguso wa kiungu kwa utukufu wa Mungu.
KUIHUBIRI INJILI YA UFALME WA MUNGU
Yesu Kristo alipoondoka hapa duniani aliacha agizo moja la msingi katika (Marko 16:15-18) \"Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa. Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya; watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.\"
Kanisa la leo linahubiri matokeo ya hilo agizo, mfano-baraka (mafanikio), na karama za Roho Mtakatifu- mfano (Uponyaji, miujiza na unabii), badala ya kuhubiri agizo lenyewe,halifahamu hiyo injili (habari njema) tuliyoagizwa kuihubiri ni ipi? Matokeo yake limehubiri Injili nyingine na kujiweka chini ya laana (Wagalatia 1:6-9) ambayo baadhi ya matokeo yake ni kuharibika kwa afya ya akili na mwili (magonjwa), kuvunjika kwa mahusiano (ndoa) na hali ngumu ya kiuchumi (umaskini).
Katika kitabu hiki utajifunza mambo ya msingi katika UFALME WA MUNGU, mfano, hiyo Injili (habari njema) tuliyoangizwa tuihubiri ni ipi?Wokovu,ujazo wa Roho Mtakatifu, uwepo wa Mungu, karama za Roho Mtakatifu, imani, mamlaka ya anayeamini, maombi, utumishi, mahusiano nk.
Kila mwana wa Mungu atakapofanyia kazi mapenzi Mungu makamilifu kama Yesu ( Yohana 4:31-34, 6:35-40, 17:4,) Mtume Paulo ( Waefeso 1:1), (Wagalatia 1:1), na mfalme Daudi (Matendo 13:36), ndipo kanisa litakuwa na nguvu kama kanisa la mwanzo lililokuwa chini ya Mitume.