INAWEZEKANA : Ujumbe Utakaokupa Kila Sababu Za Kutokata Tamaa Katika Safari Ya Kutimiza Ndoto Zako
“Ujumbe utakaokupa kila sababu za kutokata tamaa katika safari ya kutimiza ndoto zako”
Haijalishi hali au wakati mgumu unaoupitia kwenye maisha yako hivi sasa.
Iwe ni ugonjwa, Ulemavu, kufeli masomo, kukosa kazi, Biashara kufeli, kukataliwa na watu, kusalitiwa na mwenza wa ndoa n.k, Bado Inawezekana kunyanyuka tena na kusonga mbele.
Kitabu hiki kimesheheni makala zilizowasaidia wengi toka mwaka 2019 nilipoanza kuzichapisha kwenye mitandao mbali mbali ya kijamii.
Shuhuda mbalimbali kutoka Kwa watu waliozisoma na kuwasaidia wasikate tamaa kwenye maisha yao zimenipa nguvu na sababu ya kuzikusanya Kwa pamoja na kuwa kitabu Ili iwe rahisi kuwafikia na
kuwasaidia watu wengi zaidi.
Wapo wengi waliokuwa kwenye Hali ngumu kuliko unayoipitia wewe na kwa macho ya kawaida ilionekana ndio mwisho ila waliposoma maandishi haya walisimama na kusonga mbele.
Wapo waliotaka hadi kujitoa uhai ila makala hizi ziliwapa nguvu na kuwafanya waendelee kusimama wakiwa na tumaini jipya
Kila unapotaka kukata tamaa tambua zipo sababu zaidi ya milioni moja za kutofanya hivyo.
Je, unahisi kukata tamaa??Kabla ya kuchukua maamuzi hayo ya kukata tamaa soma kwanza kitabu hiki mpaka mwisho.