Your Basket

Checkout | Shopping Cart
Maisha Na Falsafa Za Safari - GetValue
Biashara & Ujasilimia Mali

MAISHA NA FALSAFA ZA SAFARI

0
0
  • 5
  • 4
  • 3
  • 2
  • 1
Price:
8,500 Tsh.
Vendor:
Added To Cart:
0
Added to shop:
Sep 30, 2023
Product Views:
585
In category:
Sample

“Maisha na Falsafa za Safari,” ni kitabu kinachoelezea safari ya maisha, changamoto mbalimbali, elimu, maarifa, ujuzi, uzoefu, kuhamasisha na kujengeana mitazamo chanya ya kukabili mambo na kusonga mbele katika kupambana kimaisha kwa matokeo chanya katika Ulimwengu huu wa kimwili na kiroho. Kitabu hiki kimegusia mambo mbalimbali katika safari hiyo, kama vile jinsi mwanadamu anavyosafiri katika safari hiyo, kuanzia kuzaliwa na kuja hapa duniani, utoto wake, kukua na ujana wake, mpaka anafikia uzeeni na kunyauka, pia changamoto mbalimbali anazokutana nazo kimaisha, imani, uchumi, ujasiriamali, utawala, maadili, malezi, makuzi, mahusiano, falsafa, elimu, ujuzi, majibu, hamasa na namna anavyokabili mazingira yake na jamii kwa ujumla.

“Maisha ni mafupi, ila yana safari ndefu ndani yake.”

“Maisha na Falsafa za Safari,” ni kitabu kinachoelezea safari ya maisha, changamoto mbalimbali, elimu, maarifa, ujuzi, uzoefu, kuhamasisha na kujengeana mitazamo chanya ya kukabili mambo na kusonga mbele katika kupambana kimaisha kwa matokeo chanya katika Ulimwengu huu wa kimwili na kiroho.

Kama ilivyo, maisha ni mafupi kwa namna ya muda tuliowekewa kuishi hapa duniani na namna ya mambo yaliyopo yanavyotukabili na kutupasa kuyatimiza kwa wakati. Wengine hudiriki kusema kuwa, “Muda hautoshi,” hasa kwa wale wengi walio na matumaini; yaani mambo ni mengi, lakini muda ni mchache huku tukizidi kunyauka.

Ila pia, pamoja na ufupi huo wa maisha, lakini ukija kuangalia namna ya baadhi ya mambo yalivyo magumu, pamoja na changamoto na mataabiko yaliyopo kwa baadhi ya watu, hufanya safari hii kwa wengine kuonekana ni ndefu sana, tena yenye dhiki na mataabiko, na kufikia kusema kuwa, “Muda hauendi, dunia imesimama na kuwaelemea,” hasa kwa wale waliokata tamaa na kupoteza matumaini.

Kitabu hiki kimegusia mambo mbalimbali katika safari hiyo, kama vile jinsi mwanadamu anavyosafiri katika safari hiyo, kuanzia kuzaliwa na kuja hapa duniani, utoto wake, kukua na ujana wake, mpaka anafikia uzeeni na kunyauka, pia changamoto mbalimbali anazokutana nazo kimaisha, imani, uchumi, ujasiriamali, utawala, maadili, malezi, makuzi, mahusiano, falsafa, elimu, ujuzi, majibu, hamasa na namna anavyokabili mazingira yake na jamii kwa ujumla.

Ni maneno yenye kufunza, kutoa elimu, maarifa, hekima, ujuzi, falsafa mbalimbali, kuhamasisha, kutia moyo na kutupatia ufunuo, taswira na dira mpya kimtazamo katika kukabiliana na mazingira yetu kimaisha, na kisha kusimama imara na kusonga mbele.

More Products On Discount
98,000 Tsh. 60,000 Tsh.

Sold by: Prophet Pd John

10,000 Tsh. 9,000 Tsh.

Sold by: Godius Rweyongeza

10,000 Tsh. 7,000 Tsh.

Sold by: Godius Rweyongeza

7,000 Tsh. 2,999 Tsh.

Sold by: Said Maumba

3,999 Tsh. 1,999 Tsh.

Sold by: Daudi Lubeleje

Best Sellers List
Best Seller
2,000 Tsh.
(5.4)

Sold by: Gaston Ngailo

Best Seller
10,000 Tsh.
(69.8)

Sold by: Samuel Macha

Best Seller
3,000 Tsh.
(16.4)

Sold by: ABDULKADIR MASSA

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PETER TARIMO

Best Seller
4,000 Tsh.

Sold by: Mashaka Khamis

GetValue Recommendations
5,000 Tsh.
(0.6)

Sold by: Denis Mpagaze

10,000 Tsh.
(1)

Sold by: PJ PROJECTS

12,000 Tsh.

Sold by: Germano Mbelwa

5,000 Tsh.

Sold by: Sabas Patrick

25,000 Tsh.

Sold by: PJ PROJECTS

Old is Gold