UJASIRIAMALI NI TABIA
UJASIRIAMALI NI TABIA; Yeyote Anaweza Kujifunza
Pamoja na uwepo wa shughuli nyingi za uzalishaji mali zinazoanzishwa na watu mbalimbali kwa lengo la kuongeza kipato chao, tafiti zinaonyesha kuwa shughuli nyingi miongoni mwa shughuli hizo hufa na kupotea katika kipindi kifupi baada ya kuanzishwa. Hata hivyo miongoni mwa shughuli chache zinazodumu, baadhi yake hushindwa kupanuka na kujiboresha katika kiwango cha kuridhisha. Moja ya sababu zinazochangia kufa au kudumaa kwa biashara mbalimbali ni wamiliki wake kukosa stadi na maarifa muhimu katika uendeshaji wa shughuli hizo. Hii inaashiria kuwa malengo ya watu wengi hayafikiwi kutokana na kukosa maarifa na stadi muhimu zinazohitajika katika uendeshaji wa shughuli zao za kiuchumi.
kitabu hiki kina lenga kutatua hizi changamoto zote............!