MAISHA NA MAFANIKIO KATIKA SANAA YA MUZIKI
JINSI YA KUFANIKIWA KATIKA MUZIKI NA SANAA KWA UJUMLA. Kama ilivyo katika maisha ya kila binadamu huwa na ndoto ya kufanikiwa na kuwa na maisha mazuri hapa duniani, tumeona watu wengi kutoka katika maisha ya chini wakifanikiwa kupitia katika shughuli mbalimbali, zikiwemo biashara, ujasiliamali na hata kuajiriwa na taasisi mbalimbali pamoja na serikali, mbali na hivyo kuna watu wamefanikiwa katika shughuli za sanaa na muziki mfano; Jay z, Kanye West, Bob Marley, Michael Jackson, Ambwene Yesaya (A.Y), Hamisi Mwijuma (Mwana FA), Naasib Abdul (Diamond Plutnumz) Ally Kiba na wengine wengi kote. Kwahiyo muziki ni biashara kama ilivyo biashara yoyote ambayo mtu humwezesha kujipatia kipato kupitia biashara hiyo, mwanamuziki hujipatia kipato kutokana na kuuzwa kwa kazi zake, maonesho na hata kutangaza biashara za makampuni na taasisi. Kwahiyo mwanamuziki hupata pesa nyingi kupitia maduka ya kimtandao ambayo huuza kazi zake duniani kote na kupata faida kama ilivyooneshwa katika sehemu ya kwanza ya kitabu hiki.
Wasanii wengi
hupendelea kufanya ushirikiano na wasanii wengine hii inaweza kuwa ndani ya
nchi au msanii kutoka nje ya nchi, hufanya hivi ili kuongeza wateja na
mashabiki katika kazi zao.
Kwa kutambua
muziki ni biashara ni muhimu zaidi kuzingatia ubora wa bidhaa sokoni na hasa
kuwa na bidhaa nyingi sokoni (Album) hii itakufanya kuwa na kazi nyingi
masikioni mwa hadhira na kukupa muda wa kutengeneza kazi zingine nyingi na
kupanua wigo wa soko lako kidunia.