MAMBO 7 USIYOYAJUA KUHUSU DHAMBI
Si kwa bahati mbaya kitabu hiki kimekufikia. DONDOO KUHUSU DHAMBI ni kitabu kwa kila mwamini kukisoma. Baada ya kusoma kitabu hiki ni matumaini yangu kupitia dondoo hizi, utapata majibu ya swali hili “Kwanini yatupasa kutunza utakatifu?” Hivyo utaongeza bidii yako kumpendeza Mungu katika mwenendo wako wote.
Si
kwa bahati mbaya kitabu hiki kimekufikia. DONDOO KUHUSU DHAMBI
ni kitabu kwa kila mwamini kukisoma. Baada ya kusoma kitabu hiki ni matumaini
yangu kupitia dondoo hizi, utapata majibu ya swali hili “Kwanini
yatupasa kutunza utakatifu?” Hivyo utaongeza bidii
yako kumpendeza Mungu katika mwenendo wako wote.
Kuokoka
ni hatua ya kwanza kuliishi kusudi lako. Dhambi ni kikwazo cha kwanza kuharibu
kusudi la Mungu katika maisha yako. Basi, kitabu hiki kiwe msaada kwako
kuongeza chachu ya wewe kutunza kusudi la Mungu kwa kuepuka kuchafuliwa na
dhambi, Kumbuka Neno la Mungu lasema “Msishike, msionje, msiguse” [Wakolosai 2:21]