
CHOCHEA KIPAJI CHAKO
Kitabu hiki ni nyenzo muhimu kwa mtu mwenye kipaji. Zipo kanuni na mbinu muhimu za kumsaidia kila mwenye kipaji kufanya vizuri sokoni. Pesa hufuata harufu ya ubora. Ukifanya kwa ubora kwenye kipaji chako lazima watu wanaofaidi kipaji chako wakulipe vizuri. Tatizo ni kwamba ubora hauji kimiujiza, bali ni matokeo ya kutumia kanuni sahihi na mbinu zilizo bora. Basi, kitabu hiki ni lazima kwako kukisoma ili ufaidike na maarifa yaliyo ndani yake.
Kitabu hiki
ni nyenzo muhimu kwa mtu mwenye kipaji. Zipo kanuni na mbinu muhimu za
kumsaidia kila mwenye kipaji kufanya vizuri sokoni. Pesa hufuata harufu ya
ubora. Ukifanya kwa ubora kwenye kipaji chako lazima watu wanaofaidi kipaji
chako wakulipe vizuri. Tatizo ni kwamba ubora hauji kimiujiza, bali ni matokeo
ya kutumia kanuni sahihi na mbinu zilizo bora. Basi, kitabu hiki ni lazima
kwako kukisoma ili ufaidike na maarifa yaliyo ndani yake.
Mara nyingi
wanaobaki kwenye ushindani na kuendelea kufanya vizuri ni wale wanaopata mbinu
mpya katika maeneo ya vipaji vyao. Ndani ya kitabu hiki zimeelezwa njia za 4
kugundua kipaji chako na haijaishia hapo, Pia kuna mbinu za kuchochea kipaji
chako baada ya kukigundua. Mbinu 5 muhimu zilizoelezwa ni;
·
Badili chanzo chako cha taarifa
·
Badili watu unaombatana nao
·
Ongeza maarifa/ujuzi
·
Jiandae nyuma ya pazia
·
Maombi
Usiache
kutumia kipaji chako. Usiache kuchochea kipaji chako. Jambo la muhimu zaidi,
kipaji chako kisikutoe kwa Mungu. Unaposoma kitabu hiki utagundua kwamba,
mwandishi anaweka mkazo, kuchochea kipaji chako huku uhusiano wako na Mungu
ukiimarika zaidi.