MEZA YA THAMANI
Price:
10,000 Tsh.
Vendor:
Added To Cart:
0
Added to shop:
Jun 30, 2026
Product Views:
16
Sample
Product Summary \\r\\nMwongozo wa kivitendo kutoka kwa mtaalamu wa HR na elimu ya fedha unaokufundisha jinsi ya kugeuza maarifa, vipaji, na uzoefu wako kuwa suluhisho linalolipa sokoni. Kitabu hiki kinakusaidia kuacha kuwa mlaji na kuwa mzalishaji wa thamani.
Product Description (Maelezo ya Bidhaa)
Umeanzisha biashara, unaomba kazi, au unatafuta mbia? Kuna swali moja gumu ambalo huamua hatima yako: \\\"Unaleta nini mezani?\\\"
Watu wengi wenye vyeti vizuri na vipaji vikubwa hukosa fursa, sio kwa sababu hawana uwezo, bali hawajui jinsi ya kufungasha (package) thamani yao kama suluhisho linaloweza kununulika. Umaskini mkubwa sio ukosefu wa pesa, bali ni ukosefu wa uwezo wa kugeuza maarifa yako kuwa sarafu inayotambulika sokoni. Dunia haina upungufu wa fursa, ina upungufu wa watu wanaojua kuleta thamani mezani.
Kupitia kitabu hiki, mtaalamu wa Rasilimali Watu (HR) na mkufunzi wa elimu ya fedha anakushika mkono kukufundisha:
- Kugundua na Kufungasha: Jinsi ya kuweka vipaji vyako katika mfumo unaonunulika.
- Weledi na Nidhamu: Mbinu za kujenga viwango vya juu vitakavyofanya soko likutafute badala ya wewe kulisaka.
- Mifumo ya Kifedha: Jinsi ya kutengeneza mifumo inayokunufaisha kifedha huku ukiwa suluhisho kwa jamii yako.
Kumbuka: Sio kila kipaji kina thamani sokoni. Thamani huanza pale ambapo kipaji chako kinatatua tatizo. Karibu kwenye meza, jifunze kuzalisha thamani inayolipa.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Godius Rweyongeza
Sold by: Lackson Tungaraza