NIDHAMU
Nidhamu ni nguzo muhimu na ya kipekee kuwezesha mtu yeyote kusonga mbele, kufanikiwa na hivyo kukomesha hali ya kukwama, kushindwa na kudumaa kukoma.\\\\\\\\\\\\\\\\r\\\\\\\\\\\\\\\\n\\\\\\\\\\\\\\\\r\\\\\\\\\\\\\\\\n\\\\\\\\\\\\\\\\r\\\\\\\\\\\\\\\\nKila anayefanya vizuri maishani ni lazima azingatie kwa umakini nguzo hii na kadri inavyokuwa imara kwako ndivyo unavyostawi na kudumu katika mafanikio. Kukosa ujenzi akinifu wa nguzo hii imefanya mafanikio ya wengi kuanguka na kuwa watu wa hadithi za nyuma yaani kipindi kile tulikuwa tunafanya vizuri na hivyo kupelekea kukosa mguso endelevu katika jamii inayowazunguka.
KUHUSU KITABU
Nidhamu ni daraja la kukuvusha kutoka pale ulipo na kule unapoelekea kuitwapo Mafanikio. Kesho yako ni Leo inayotekelezwa kwa vitendo na kwa kudhamiria. Ni kweli unamwamini Mungu kujionea ustawi na mafanikio, bali pasipo ujenzi thabiti wa nguzo hii hupelekea maisha kuonekana ni ubatili mtupu.
Nidhamu ni chungu wakati wa utekelezaji bali unapoendelea kujihusisha katika ujenzi wake hupelekea mambo makuu kutokea yenyewe ikiwemo mgeuko wa fikra, ongezeko la thamani yako na ubora katika kuwasilisha unachokifanya.
Wengi tunatamani heshima bila utayari wa kulipa gharama ya ujenzi wa nguzo hii ya nidhamu. Katika kila eneo la maisha nidhamu ni kiini cha uendeshaji na kuwezesha kufikia malengo husika kama mtu binafsi, familia na taasisi. Yamkini una ndoto, maono au kusudi unatarajia kwa dhati uone ukamilifu wake lakini pasipo nidhamu ni sifuri.
Watu wote mahiri katika eneo lolote iwe ni elimu, sanaa, sayansi, uchumi, au mambo ya kiroho na kijamii ni mrejesho kuwa kuna nidhamu wanaihusisha kila wakati kuwafanya wakipekee na kuleta mguso katika jamii.
Mikakati na malengo pasipo nidhamu ya utekelezaji ni sawa na kujilisha upepo.Hatima za wengi zimeishia njiani na kushindwa kutimia kwa kukosa nguzo hii ya nidhamu.
Kitabu Hiki ni mahsusi kwa wale tu ambao wamechoka ukawaida na wanataka kuchochea asili ya mambo yasiyo ya kawaida kwa kudhamiria kuhusisha nidhamu ya kutekeleza kila mpango, agenda na kuishi maisha yenye utaratibu kwani kuishi bila utaratibu ni kujiharibu pasipo kujua.
Chukua nakala yako sasa.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza