Your Basket

Checkout | Shopping Cart
Ongeza Kipato Chako Na Kuku Wa Kienyeji - GetValue
Biashara & Ujasilimia Mali

Ongeza Kipato Chako Na Kuku Wa Kienyeji

0
0
  • 5
  • 4
  • 3
  • 2
  • 1
Price:
12,000 Tsh.
Added To Cart:
0
Added to shop:
Jun 06, 2022
Product Views:
2,425
In category:
Sample

Ongeza Kipato Chako na Kuku wa Kienyeji ni kitabu kitakachokuvusha changamoto za ufugaji wa kuku na kukupatia njia rahisi za kuanza kuvuna pesa nyingi kupitia kuku wa kienyeji.

ONGEZA KIPATO CHAKO NA KUKU WA KIENYEJI

“Mbinu Rahisi na Haraka za Kufuga Kisasa na Kitaalamu kwa Mfugaji Anayeanza Biashara.”

Tunaishi katika kipindi ambacho bei za bidhaa zinapanda sana wakati thamani ya fedha inazidi kushuka. Kila kukicha watu wanapata hofu ya uwezo wao wa kuendelea kumudu mahitaji ya kila siku.

Utaona hata uwezo wa watu kupata mahitaji ya lazima ya maisha kama vile chakula, mavazi na makazi au malazi umepungua. Ajira zimekuwa changamoto kupatikana na zikipatikana kipato chake kinakuwa kidogo sana ambapo ni vigumu kuona unafuu wa maisha.

Hakuna mitaji. Mabenki, wafadhili, wadhamini na taasisi za kifedha zinaangalia sana usalama wa fedha zao hivyo ni vigumu kuwakopesha wajasiriamali wanaoanza.

Kutokana na changamoto hizi kuna mahitaji makubwa ya mbinu za kujikwamua katika hali hiyo. Huenda tayari hadi unaposoma hapa umejaribu njia nyingi za kujikomboa bila mafanikio.

Jamii inahitaji suluhisho rahisi kwa changamoto za ajira na hali duni ya maisha. Suluhisho ambalo litamkwamua mtu ndani ya muda mfupi bila kutumia rasilimali nyingi na ambalo litamfaa kila mtu bila kujali umri wake kwenye mazingira yote.

Suluhisho hilo ni Ufugaji wa kuku wa kienyeji. Ufugaji wa kuku wa kienyeji ni fursa kubwa ya kuongeza kipato chako na familia yako. Kila mtu kwenye kaya anaweza kunufaika kupitia mradi huu.

Ni fursa ambayo kuanzia mtoto anayesoma shule ya msingi ya kutwa au bweni hadi mtu mzee kabisa yani kikongwe anaweza kuichangamkia. Ni fursa mtambuka kwani pamoja na kuboresha chakula cha familia moja kwa moja pia inaongeza kipato cha kaya.

Kitabu cha "Ongeza Kipato Chako na Kuku wa Kienyeji" kitakupatia mbinu rahisi za haraka na kitaalamu za kufuga kuku wa kienyeji hata kama ndiyo unaanza. Lengo ni kukusaidia unayeanza ufugaji huu uufanye kiurahisi lakini upate mazao mengi kwa muda mfupi zaidi.

Kwa mfugaji wa kuku wa kienyeji kitabu hiki kitakupa mbinu za kuboresha ufugaji wako uanze kupata faida endelevu. Utaweza kupanua mradi wako uwe shughuli rasmi ya kiuchumi siyo kupata mboga ya kukarimu wageni au kama kitoweo cha sherehe na sikukuu tu.

Hiki ni kitabu ambacho kila mwana familia anatakiwa kusoma, kila kijana anayetaka kujikwamua kiuchumi, kila mtu anayejiandaa kustaafu, kila mtu anayetafuta njia ya kulipa madeni na mikopo yake, kila mtu anayetafuta mtaji wa biashara ya ndoto zake na kila mama wa nyumbani.

Ona baadhi ya shuhuda za watu waliopata maarifa ya kitabu hiki

Baraka John

“Naachana na kazi za serikali naanza kufuga kuku wa kienyeji maana nimejifunza mengi sana.”

Mutta J. Mutta

“Hakika umezidi kutonesha kidonda cha ndoto yangu maana naona kama nimechelewa sana ila naamini kwamba niungane na ndugu na wadau wengine tukuombee dua na maombi ili uendelee kutupatia zaidi madini yaliyojificha.”

Patrick Nzunda

“Mafunzo haya ni mazuri sana. Yanajenga wigo mpana wa mawazo ya kimaisha. Ningependa kujua mambo mengi. Asanteni. Mada ya ufugaji wa kuku wa kienyeji imenibariki sana.”

Ritha Msuya

“Nimevutiwa sana kwa kweli inafundisha vizuri na nimetiwa moyo sana na ninamwomba Mungu anisaidie naamini na mimi nitajiajiri kwani nimehitimu chuo mwezi wa nne sasa natumaini nimepata elimu na nitaweza kujiajiri mwenyewe.”

Sebastian Ndohelo

“Hakika somo ni zuri mno kwa mwenye nia ya dhati na aliye tayari kuzingatia maelekezo, nimetiwa moyo. Endelea kutoa elimu muhimu.”

Athumani Mohamedi

“Asante sana nimeupokea ujumbe huu kwa nia ya dhati na nimeanza kujenga mabanda kwa ajili ya mradi wa kuku wa kienyeji.”

Joseph Nelson Kambanga

“Ninapanga kuanza ufugaji wa kuku na tayari nimenunua heka 2 Wilaya ya Kisarawe kwahiyo ujumbe huu umekuwa wa msaada.”

Kitabu hiki hakiongezi orodha ya machapisho kwenye kabati lako bali kinakupa hazina ya ujuzi kichwani na pesa nyingi mfukoni kwako.

Unakosaje nakala yako? Hakikisha kitabu hiki kinafika mkononi kwako.

Imeandikwa na Mujaya Jones Mujaya ambaye ni mwandishi wa Kitabu cha “Ongeza Kipato Chako na Kuku wa Kienyeji.”

Mawasiliano: +255768678122

                        ev.mujaya@gmail.com


More Products On Discount
6,000 Tsh. 5,000 Tsh.

Sold by: Godius Rweyongeza

5,000 Tsh. 1,000 Tsh.

Sold by: RAMV MRUMA

7,000 Tsh. 2,999 Tsh.

Sold by: Said Maumba

30,000 Tsh. 20,000 Tsh.

Sold by: Lackson Tungaraza

Best Sellers List
Best Seller
10,000 Tsh.
(5.4)

Sold by: Gaston Ngailo

Best Seller
10,000 Tsh.
(69.8)

Sold by: Samuel Macha

Best Seller
3,000 Tsh.
(16.4)

Sold by: ABDULKADIR MASSA

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PETER TARIMO

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PASTOR TONY OSBORN

GetValue Recommendations
Old is Gold