SAUTI YA MWANAMKE MWENYE HEKIMA
Sauti ya mwanamke mwenye hekima (Mafunzo 17 ya maisha niliyojifunza kwa mama, maalumu kwaajili ya Binti
SAUTI YA MWANAMKE MWENYE HEKIMA
Je, unawezaje kusimama imara wakati ulimwengu wako unapotikisika?. Kitabu hiki ni safari ya kweli ya mabadiliko ya binti aliyelazimika kukua haraka kuliko umri wake pale maisha ya familia yake yalipogeuka ghafla. Kupitia sauti ya mama yake, Johanitha Jeremiah Ernest anashirikisha mafunzo 17 ya dhahabu yaliyomjenga kuwa mwanamke mwenye maono, ujasiri, na msimamo thabiti.
Ndani ya kitabu hiki utagundua, SIRI kama:
- Mungu Juu ya Yote: Jinsi ya kuishi kwa kumtegemea Muumba kama msingi wa kila kitu.
- Utambulisho Wako: Siri ya kujijua wewe ni nani na kulinda thamani yako kama binti wa kifalme.
- Nguvu ya Maombi na Sadaka: Jinsi ya kufungua malango ya baraka na kuvunja minyororo ya vizazi.
- Tabia na Utu: Kujenga vazi la kudumu la heshima ambalo sura haiwezi kukupa.
- Pamoja na mafunzo mengine ya maisha yanayolenga nyanja za aendeleo binafsi, kiroho, kiuchimi na hata malezi
Hiki si kitabu tu; ni urithi wa maisha kwa binti yeyote nanayetaka kusimama kama mshindi katikati maisha, sikia sauti ya hekima, amini uwezo ulio ndani yako, na anza kuandika hadithi yako upya leo.
"Sauti ya mama haikuishia kwenye nyumba yetu. Inaendelea kuishi ndani yangu, na sasa ndani ya kila mtu atakayesoma kitabu hiki." Johanitha Jeremiah Ernest
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza