SILAHA ZA VITA VYETU
SILAHA ZA VITA VYETU. Ingawa tunaenda kwa Jinsi ya mwili lakini hatufanyi vita vyetu kwa jinsi ya Mwili.
Moja kati ya jambo ambalo huwezi kulikwepa katika maisha yako wewe kama mkristo ni kupigana vita. Biblia inasema katika kitabu cha; Mathayo 10:16\\\\\\\"Angalieni, mimi nawatuma kama kondoo kati ya mbwa-mwitu; basi iweni na busara kama nyoka, na kuwa watu wapole kama hua.\\\\\\\" Neno hili ni uthibitisho wa kuwa sisi tumezingirwa na adui pande zote za maisha yetu. Kwenye huduma na utumishi wako utakutana na adui wanaokusubiri kukumaliza, kwenye ndoa utakutana na adui ambao wana kazi moja tu ya kuhakikisha ndoa yako inaharibika, katika biashara nako wapo adui wengi ambao wamejiandaa kukupiga. Kwahiyo kila eneo la maisha yako wapo adui ulimwengu wa roho na wa mwili ambao wamejipanga kupigana na wewe.
Sasa ili uweze kuishi maisha ya ushindi hapa duniani ni lazima ukubali kupigana vita na kushinda. Na ushindi wako unategemeana na kiwango chako cha maandalizi na uwezo wako wa kuzitumia silaha za vita zako. Kitabu hiki cha \\\\\\\"SILAHA ZA VITA VYETU\\\\\\\" ni kitabu ambacho kimeelezea kiundani juu ya; -Maisha ya mkristo na aina za vita anazokutana nazo katika maisha yake. -Sababu za mkristo kupigwa vita.
-Silaha za kutumia ili kupigana vita na adui.
-Mambo yatakayokusaidia kumshinda adui.
Mwisho wa kitabu hiki yameambatanishwa maombi ya vita ambayo yatakusaidia kukuongoza kuomba na kujitwalia ushindi wako.
Zaidi ya yote Neno la Mungu linasema kuwa; Warumi 8:37 \\\\\\\"Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.\\\\\\\" Hivyo huu ni ujasiri wetu ya kuwa katika vita zote tutakazokutana nazo katika maisha yetu sisi ni washindi.
Kwahiyo Mwanangu nenda kauchukue ushindi wako kwa jina la Yesu.
JIPATIE NAKALA NYINGINE KUTOKA KWA PASTOR TONY OSBORN
NGUVU NYUMA YA KUFUNGA NA KUOMBA https://www.getvalue.co/prod/nguvu_nyuma_ya_kufunga_na_kuomba
KUUWEZA WAKATI UJAO https://www.getvalue.co/prod/kuuweza_wakati_ujao
MATTERS OF THE BLOOD https://www.getvalue.co/prod/matters_of_the_blood
SIGNS AND TOKENS https://www.getvalue.co/prod/signs_and_tokens
KWAKUA SASA UMEOKOKA https://www.getvalue.co/prod/kwa_kuwa_sasa_umeokoka
NDOTO UANZOOTA NA UHALISIA WAKE https://www.getvalue.co/prod/ndoto_unazoota_na_uhalisia_wake
CHRISTIANS IN THE BUSINESS WORLD https://www.getvalue.co/prod/christian_in_business_world
DEALING WITH ADDICTIONS https://www.getvalue.co/prod/dealing_with_addictions