CHRISTIAN IN BUSINESS WORLD
CHRISTIANS IN THE BUSINESS WORLD.
Moja ya maswali mengi ninayokutana nayo kutoka kwa wanangu wa kiroho ni kuwa; \\\\\\\"Inawezekanaje watu wa duniani wanaonekana wana mafanikio makubwa katika kazi zao, biashara zao na maisha yao kiujumla kuliko watu ambao wanasema wanamjua Mungu?\\\\\\\" Jambo ambalo watu wengi hawalijui ni kuwa; watu wa duniani wana njia zao ambazo kwao wakizitumia katika maisha yao wanafanikiwa na sisi tuliokoka tunazo njia zetu ambazo tukizitumia tunafanikiwa pia. Neno la Mungu linasema katika kitabu cha;1 Wakorintho 10:3-4 \\\\\\\"Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; (maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;)\\\\\\\" Kwahiyo ijapokuwa tupo duniani njia zetu tunazopaswa kutumia ni tofauti na watu wa duniani.
Shida kubwa ya wakristo wengi ni kutaka kufanya biashara zao na mambo yao kama watu wa dunia hii. Kwa namna hiyo kamwe hawawezi kuona matokeo yeyote.
Kitabu hiki cha \\\\\\\"CHRISTIANS IN THE BUSINESS WORLD\\\\\\\" ni kitabu ambacho kimetoa muongozo wa kutosha wa hekima, maarifa na ufahamu wa Kimungu wa namna ya kufanikiwa kibiashara kama mkristo. Kitabu hiki kimeandika pia juu ya siri na kanuni zitakazomuwezesha mkristo yeyote kufanya vizuri katika ulimwengu wa biashara na kufikia mafanikio makubwa.
Zaidi ya yote kitabu hiki kimeambatanishwa maombi ambayo wewe kama mfanyabiashara unaweza ukayatumia kuombea biashara yako na bidhaa zako lakini pia Kuna mkusanyiko wa matendo ya kiimani (signs and tokens) ambazo nazo zitakusaidia kupata matokeo mazuri katika biashara zako.
Neno la Mungu linasema katika kitabu cha Hagai 2:8 \\\\\\\"Fedha ni mali yangu, na dhahabu ni mali yangu, asema BWANA wa majeshi. Hivyo wewe kama mtoto wa Mungu ni haki yako kufanikiwa katika kila unachofanya. Mimi kama mchungaji wako ninakuombea Mungu akakusaidie na kuendelea kubariki kazi za mikono yako siku zote, Amen.
JIPATIE NAKALA NYINGINE KUTOKA KWA PASTOR TONY OSBORN
NGUVU NYUMA YA KUFUNGA NA KUOMBA https://www.getvalue.co/prod/nguvu_nyuma_ya_kufunga_na_kuomba
SILAHA ZA VITA VYETU https://www.getvalue.co/prod/silaha_za_vita_vyetu
KUUWEZA WAKATI UJAO https://www.getvalue.co/prod/kuuweza_wakati_ujao
MATTERS OF THE BLOOD https://www.getvalue.co/prod/matters_of_the_blood
SIGNS AND TOKENS https://www.getvalue.co/prod/signs_and_tokens
KWAKUA SASA UMEOKOKA https://www.getvalue.co/prod/kwa_kuwa_sasa_umeokoka
NDOTO UANZOOTA NA UHALISIA WAKE https://www.getvalue.co/prod/ndoto_unazoota_na_uhalisia_wake
DEALING WITH ADDICTIONS https://www.getvalue.co/prod/dealing_with_addictions