30 Secret Keys To The Best
Ni wengi wanatamani kufanikiwa na kuwa Bora katika maisha, Lakini ni wale tu wanaojua siri na kuziishi ndio hufanikiwa na kuwa Bora maishani.
"Success is never a surprise it's a decisive process"
Mafanikio yoyote ni mchakato, Wala sio ndoto ya Siku moja tu (a day dream). Kila aliyefanikiwa nyuma yake Kuna mchakato ameupitia ambao ulimgharimu muda mwingi wa kufanya bila kuchoka, kufanya kwa muendelezo, na kufanya zaidi ya kawaida
Mafanikio ya mtu huamuliwa n akiwango chake Cha maarifa katika eneo husika, huwezi kufanya kitu zaidi ya unavyoweza n aunavyofahamu jinsi ya kufanya. Kiwango Cha maarifa ndani yako kitamaua wewe uwe ufanikiwe na kuwa Bora kwa kiwango gani.
Kiwango Cha maarifa ndani yako huwa hakiji hakijitokezi tu Kama ajali Wala huzaliwi nacho, Ni swala la maamuzi ya kujifunza kila siku kwa namna mbalimbali ambazo zitakupatia maarifa sahihi yatalayokusaidia kukua na kuimarika katika eneo husika.
Kuwa Bora Ni zaidi ya kufaulu, kwani unaweza kufaulu lakini kwa kiwango Cha wastani yaani mtu wa kawaida (average person), lakini kuwa Bora ni kuwa chagua la kwanza katika mengi mazuri.
Unaweza kuwa Bora katika mtazamo wa watu wakikulinganisha na Wengine katika unachofanya, lakini pia unaweza kuwa Bora katika uwezo(potential) wako mwenyewe ukilinganisha matokeo yako na uwezo wako wa utendaji kazi katika eneo hilo.
Kuwa Bora sio Jambo la kubahatisha au bahati nasibu, Ni swala la mamauzi na hatua za kimkakati
"Excellence is never an accident, it's a strategic decion"
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza