Binti Rhobi : Malaika Wa Zamu
Waliua mpenzi wake mbele yake na kumwambia sahau. Leo amerudi sio kama mwanamke, bali kama Malaika wa Zamu. Damu kwa damu.
Kwa pumzi ya mwisho "Walinifanya mjane kabla hata sijawa mke." Binti Rhobi alipoteza kila kitu siku moja. Mpenzi wake wa maisha aliuawa kikatili mbele ya macho yake na watu wenye pesa na nguvu. Alienda mahakamani kutafuta haki, mahakama ikambebesha msalaba. Alienda jijini kulia, kijiji kikamcheka. Sasa miaka 4 baadaye, jijini kuna tetesi ya mwanamke mrembo anayevaa vazi jeupe usiku na anamvuto wa mithili ya malaika. Anaitwa MALAIKA WA ZAMU. Analipiza kisasi kwa kila mtu aliyehusika kwenye kifo cha mwanaume wake. Mmoja baada ya mwingine. Utapata nini ndani ya hadithi hii?
1. Mapenzi mazito yatakayokutoa machozi
2. Usaliti na hila za marafiki
3. Kisasi kitamu ambacho hakijawahi kuandikwa
4. Mwisho usiotarajiwa utakao kuacha mdomo wazi Hii sio hadithi ya kulia.
Ni hadithi ya mwanamke aliyeamua kuwa mkatili kuliko wale waliomuulia mwanaume wake.