Your Basket

Checkout | Shopping Cart
Fahamu Misingi Na Kanuni Za Ndoa - GetValue
Biashara & Ujasilimia Mali

FAHAMU MISINGI NA KANUNI ZA NDOA

0
0
  • 5
  • 4
  • 3
  • 2
  • 1
Price:
10,000 Tsh.
Vendor:
Added To Cart:
0
Added to shop:
Jun 22, 2025
Product Views:
13
In category:
Sample

Mwongozo Wa Kujenga Mahusiano Ya Kudumu.

Najua utakuwa umeshawahi kujiuliza, kwa nini mahusiano ya ndoa nyakati hizi yamekuwa na changamoto nyingi sana? Kwa nini ndoa za wazazi wetu zimeendelea kudumu miaka na miaka tofauti na mahusiano ya ndoa kwa vizazi vya hivi karibuni? Majibu yake ndio yakanifanya niandike kitabu hiki ambacho kitaweka nuru na dira katika mchakato wa mahusiano ya urafiki, uchumba hadi kupelekea ndoa zenye uimara.

Ukweli ni kuwa siku za hivi karibuni kumekuwa na changamoto kubwa katika mahusiano hasa katika ndoa kiasi kwamba kumekuwa na matokeo ya vifo baina ya wanando. Je, ni kweli mahusiano ya ndoa yamekuwa na changamoto kubwa kiasi hicho hadi kufikia watu wawili hapo mwanzo waliopendana sana kuuana? Baada ya kutafakari sana nikaona nikuandikie habari za mahusiano ya NDOA ili walau uchukue tahadhari mapema pindi unapokumbana na changamoto za mahusiano ya ndoa.


Nimeamua kuandika kitabu hiki kwa ajili ya wale wote wanaojitayarisha kufunga ndoa, wale walio kwenye ndoa tayari, na kwa yeyote anayetamani kupata ufahamu zaidi kuhusu maisha ya ndoa. Kwa sababu tunaishi katika siku ambazo talaka zimekuwa nyingi na utata mwingi kuhusu suala hili, wengi wanaogopa hata kuanza hadithi zao za ndoa. Kuna watu wengi wanaohisi kwamba wamenaswa kati kati ya sura ya mahusiano yao ya ndoa wasizozipenda. Nisingependa ukifunge kitabu cha

ndoa yako mapema kama wengi wanavyoendelea kufanya. Nataka nikusaidie ufungue ukurasa mpya. Pia kuna wengi wasioweza kuhesabika walioamini kwamba hadithi za mahusiano yao ya ndoa hazingewahi kuisha, kuna walioshtukia mapema

kwamba kurasa za mahusiano yao katika ndoa zimeraruliwa ghafla kutoka kwenye maisha yao na talaka au kifo cha wenza wao. Naomba niwatie moyo kuwa bado hadithi zao za maisha ya ndoa hazijaisha.


Ukweli ni kuwa wengi wetu tulijengewa mawazo kuwa maisha ya ndoa ni ya matatizo tu, naamini hata leo hii bado wengi wanafikiri hivyo, wamepokea hivyo, ndio maana kila anayeoa au kuolewa lazima aambiwe kuwa nenda kavumilie. Sijui wewe uliambiwaje? Watu wengi wanatiana moyo utasikia wakisema, “jipe moyo mpendwa hilo ndilo jaribu lako”. Utafikiri kweli Mungu ndio kalipanga hilo jaribu, sikiliza, si mpango wa Mungu ndoa iwe sehemu ya mateso au iwe ni sehemu ya matatizo yanayopelekea watu kukosa amani na hata kupata magonjwa na kufa au kushindwa kumtumikia Mungu wao.

HIVYO BASI...

Ni tumaini langu kupitia kitabu hiki nitaweza kukusaidia kuchochea imani yako na uhakika wa maisha mazuri yenye upendo kwa wale ambao bado hawajaanza safari ya ndoa na wale walio tayari katika ndoa. Nakutia moyo tena kuwa inawezekana tena kutengeneza upya hadithi yako nzuri katika maisha ya ndoa kwani NDOA NI MPANGO ASILI WA MUNGU!





More Products On Discount
Best Sellers List
Best Seller
1,000 Tsh.
(5.4)

Sold by: Gaston Ngailo

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PASTOR TONY OSBORN

Best Seller
10,000 Tsh.
(69.8)

Sold by: Samuel Macha

Best Seller
3,000 Tsh.
(16.4)

Sold by: ABDULKADIR MASSA

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PETER TARIMO

GetValue Recommendations
Old is Gold