Falsafa Za Majuha
Falsafa Za Majuha
Joseph Masalu anakutana na rafiki yake Paul Makala wakati akihangaika kujisajili kwa ajili ya masomo ya mwaka wa kwanza katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kutokana na kupangwa katika chumba kimoja bwenini, usahibu wa marafiki hawa waliofahamiana tangu enzi za masomo ya shule ya upili unaota na kukita mizizi katika nafsi zao. Katika hafla ya kuwakaribisha wanachuo kikuu wa mwaka wa kwanza, Makala anakutana na binti anaefahamika kwa jina la Lucy na kujenga nae urafiki.
Baada ya mwaka wa kwanza wa masomo; kwa siri, Lucy anatoka katika hosteli za chuo na kwenda kuchimba kaburi maeneo ya Changanyikeni. Hawa anamsaidia Makala kuona kaburi hilo. Baada ya kuliona, Makala anafadhaika na kuamua kukata vipande vidogo vidogo vya sonona yake na kumgawia kila mwanachuo kikuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam! Ungana na wanachuo kikuu muende kutazama ‘Gimba lisilo roho.’
J.P Makula ni mwanafasihi nguli aliyekuwa hana jina hadi alipokamilisha mswada wa riwaya hii. Kitaaluma ni mwalimu wa masomo ya lugha (Kiswahili na Kingereza.)