Ifahamu Saratani Ya Matiti
“Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Hosea 4:6”
Kukukosekana kwa ufahamu, maarifa na taarifa sahihi kuhusu magonjwa mbalimbali haswa yasiyo ya kuambukizwa ni jambo linalosababisha madhara zaidi katika jamii zetu, kwani kwa kuto kufahamu watu hupuuza au kubedha dalili za awali za magonjwa hayo, hivyo kushindwa kuutambua ugonjwa mapema wakati ambapo matibabu yake yanaweza kutekelezeka kwa mafanikio zaidi.
Mambo mbalimbali yanaweza kuwa sababu ya watu kutokupata taarifa sahihi au zisizo kamili, ikiwemo: kutokupata nafasi ya kupokea elimu mojakwamoja kutoka kwa wahudumu wa afya, kushindwa kufanya uchaguzi sahihi wa taarifa kwa watu wanao soma mitandaoni, tatizo la lugha; taarifa nyingi katika vitabu na mitandaoni mara nyingi huwa zipo katika lugha ya kiingereze pia tabia ya kutokupenda kusoma kabisa.
Kitabu hiki kimekusanya taarifa muhimu kuhusu saratani ya matiti; ni nini, dalili zake ni zipi, inasababishwa na nini, namna unavyoweza kupunguza hatari ya kupata saratani ya matiti na matibabu yake. Yote yamewekwa katika lugha lahisi kuelewa kwa yeyote anayeweza kusoma Kiswahili.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza