
Itambue Nguvu Ya Sadaka Na Siri Ya Utoaji
K\\\\\\\\r\\\\\\\\natika maandiko matakatifu, sadaka na utoaji vimepewa nafasi ya kipekee kama sehemu ya ibada na kipimo cha imani ya mtu kwa Mungu. Tangu Agano la Kale hadi Agano Jipya, tunaona kuwa Mungu amekuwa akiweka baraka, ulinzi, na mawasiliano ya kipekee kati yake na mwanadamu kupitia moyo wa kutoa. Biblia inasema:\\\\\\\\r\\\\\\\\n\\\\\\\\r\\\\\\\\n“Wapeni, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa, kushindiliwa, kusukwasukwa na kumwagika, watamwaga katika vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.” Luka 6:38\\\\\\\\r\\\\\\\\nSadaka si tu tendo la kutoa mali, bali ni ushuhuda wa moyo wa kumtumainia Mungu kuliko vitu. Kupitia kitabu hiki, msomaji atafundishwa si tu kuhusu aina za sadaka, bali pia siri zilizofichika ndani ya utoaji unaofanyika kwa moyo wa ibada, utii, na upendo.\\\\\\\\r\\\\\\\\n\\\\\\\\r\\\\\\\\nBiblia pia inasema:\\\\\\\\r\\\\\\\\n “Heri mtu yule amchukiaye Mungu, afanyaye mapenzi yake; yeye hueneza, huwapa maskini; haki yake hudumu milele.” Zaburi 112:1, 9\\\\\\\\r\\\\\\\\n\\\\\\\\r\\\\\\\\nSadaka huenda mbali zaidi ya kutoa mali—huleta mvuto wa kiroho, hupenya mbingu, na kuamsha rehema za Mungu. Ibrahimu alitoa, Mungu akafanya agano naye. Sulemani alitoa, Mungu akamjibu kwa ndoto ya hekima. Kanisa la Makedonia lilitoa kwa moyo wa hiari hata katika hali ya umaskini, na Mungu aliwatangaza kuwa kielelezo cha neema ya utoaji.\\\\\\\\r\\\\\\\\n\\\\\\\\r\\\\\\\\nKitabu hiki kimeandikwa ili kuamsha uelewa wa kiroho kuhusu sadaka kama silaha ya ushindi, mlango wa baraka, na daraja la kumkaribia Mungu. Siri za utoaji zilizofichwa kwa wengi, zitafunuliwa hapa kwa msaada wa Neno la Mungu, ili kila msomaji aweze kutembea katika njia ya baraka isiyoisha.\\\\\\\\r\\\\\\\\n\\\\\\\\r\\\\\\\\n“Mtu mkarimu atabarikiwa, kwa kuwa huwapa maskini chakula chake.” Methali 22:9\\\\\\\\r\\\\\\\\n\\\\\\\\r\\\\\\\\nKaribu katika safari ya kiroho, safari ya kugundua kwamba sadaka yako si ya kawaida—ni mbegu ya muujiza wako.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza