Ndoto Ya Kweli Haifi
Ndoto Ya Kweli Haifi
Ni asubuhi yenye kupendeza jua likiwa limechomoza kuashiria siku mpya imewadia Noela aliamka na kujinyoosha akiwa ametoka katika nyumba ya nyasi aliinamisha mgongo kutoka ndani huku akipikicha macho mawazo yakiwa yametawala akili yake. ‘’Lini mimi nitatoka kwenye maisha kama haya kula shida kulala shida?’’ alikuwa akijiuliza mwenyewe alitamani kuondoka kijijini Bariadi kwenda katika mji wa Mwanza hakutamani kuendelea kuishi maisha ya pale kijijini Bariadi kilichokuwa Mkoa wa Simiyu. ‘’Noela noela?’’ aliita Mama yake Mkubwa ambae aliishi nae nyumbani, ‘’Abee mama mkubwa’’ Mama yake mkubwa alisimama kutoka katika ngozi waliokuwa wamelalia sakafuni akamsogolea Noela mlangoni. ‘’Sasa noela tukakate kuni ili tuje kupika uji’’ alisema Mama yake mkubwa na Noela ‘’uji na unga haumo si unakumbuka jana tulilala njaa!’’ anaongea kwa uvivu Noela, ‘’hapana nitaenda kuomba kwa mama….’’ Noela alikuwa hapendi maisha ya kuomba hata kama angekuwa na maisha magumu kiasi gani, endelea............!
Sold by: Godius Rweyongeza
Sold by: Lackson Tungaraza