FAIDA NA HASARA ZA KIFO
MAISHA NI SAFARI\r\nUmewahi kusikia neno hili ya kuwa maisha ni safari? Mimi nimewahi kulisikia tena mara nyingi mno, bila shaka hata wewe umelisikia lakini nikuulize swali je? wanaposema maisha ni safari huwa wanamaanisha nini? Ukweli ni kuwa huwa wanamaanisha tupo safarini, lakini je? tunasafiri kwenda wapi? Hakika tunasafiri kuelekea kifo. Ndiyo maana kuna wengine husema tunaishi tunaishia. Ni vizuri sana kujua kwamba tuko safarini hivyo hakuna safari isiyo na maandalizi. Ni shetani asiyetaka watu kufikiri kuwa ipo siku tutaondoka duniani, hii ni kwasababu hataki watu wajiandae na safari hiyo ya kifo lakini nakusihi wewe usimuunge mkono shetani na wazo lake hilo. \r\nTena katika safari hiyo ya kuishi, mwanadamu mmoja huishia kwa kupata faida ya kifo na mwingine huishia kupata hasara, sawa na kila mmoja alivyochagua kutembea hadi mwisho wa safari yake.\r\nHebu twende moja kwa moja kufahamu kwanza Kifo ni nini? \r\nKIFO NI NINI?\r\nKifo ni ile hali ya mwili kutengana na roho. \r\nYakobo 2:26 “Maana kama vile mwili pasipo Roho umekufa”\r\nBiblia imetupa tafsiri rahisi ya neno kifo, aaah ni tafsiri nzuri na ya kweli kabisa. \r\nKabla mwanadamu yeyote kuzaliwa alitokea katika hali ya kifo au kwa lugha nyepesi alikuwa amekufa hii ni kutokana na tafsiri ya neno la Mungu kutoka katika kitabu cha Yakobo. \r\nMaana yake kabla haujafika duniani haukuwa na mwili hivyo roho yako na mwili wako vilikuwa vimetengana. Na hii inathibitishwa katika maandiko ya kitabu cha Mwanzo wakati Mungu alipokuwa akikamlisha kazi ya uumbaji wa mtu kwa kuunganisha mwili wake na roho na hapo ndipo mtu akawa nafsi hai, baada ya kupuliziwa pumzi ya uhai, kumbe kabla ya hapo hakuwa hai.\r\nMwanzo 2:7 “Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi akampulizia puani pumzi ya uhai mtu akawa nafsi hai”
\r\n\r\nKifo ni ile hali ya mwili kutengana na roho.
Yakobo 2:26 “Maana kama vile mwili pasipo Roho\r\numekufa”
Biblia imetupa tafsiri rahisi ya neno kifo, aaah!! ni tafsiri nzuri na ya kweli kabisa.
Kabla ya mwanadamu yeyote kuzaliwa alitokea katika hali ya kifo au kwa lugha nyepesi alikuwa amekufa hii ni kutokana na tafsiri ya neno la Mungu kutoka katika kitabu cha Yakobo.
Maana yake kabla haujafika duniani haukuwa na mwili hivyo roho yako na mwili wako vilikuwa vimetengana. Na hii inathibitishwa katika maandiko ya kitabu cha Mwanzo wakati Mungu alipokuwa akikamlisha kazi ya uumbaji wa mtu kwa kuunganisha mwili wake na roho na hapo ndipo mtu akawa nafsi hai, baada ya kupuliziwa pumzi ya uhai ndipo akawa kiumbe hai kumbe! kabla ya hapo hakuwa hai katika mwili.
Mwanzo 2:7 “Bwana Mungu akamfanya\r\nmtu kwa mavumbi ya ardhi akampulizia puani pumzi ya uhai mtu akawa nafsi hai”