Jiandae Kuishi
Wewe JE? Utafanya nini baada ya kuufikia ukomo wako wa kuwepo shuleni / kazini? Utafanya nini, ukifukuzwa kazi unayoifanya sasa? Utafanya nini mwili wako utakapokuwa hawezi? Utakuwa nani /utaishi na nani/ utaonekanaje baada ya nafasi uliyonayo kufika tamati? Utakuwa mgeni wa NANI.
Katika kila sehemu utakayo kuwepo kwa wakati fulani wa maisha yako, lazima utafika muda ambapo itakulazimu kuondoka; iwe kwa heri, au kwa shari:
- Kama mwanafunzi ikosiku uanafunzi wako utakoma
- Kama mfanyakazi, ikosiku ajira yako itakoma
- Kama kiongozi, ikosiku uongozi wako utafikia tamati
- Kijana mwenye nguvu, ikosiku utakuwa huwezi
- Ni busara kuyatambua haya mapema ....
… 3 Yule karani akafikiri: ‘Bwana wangu amenifukuza kazi ya ukarani; nitafanya nini? Kwenda kulima siwezi; kwenda kuombaomba kama maskini ni aibu. 4Naam, najua la kufanya, ili nitakapofukuzwa kazi, watu waweze kunikaribisha nyumbani kwao...’ Luka 16: 1-9.
Karani dharimu aliutambua wakati wa ukomo wakazi yake ya ukarani, akajiuliza nini atafanya ili kuishi baada ya kukoma kwa kazi yake? Akatafuta na akapata majibu aliyoyaona kuwa ni sahihi na yanaeza kumsaidia. Hakuishia hapo, akaanza kuyafanyia kazi majibu yake wakati huohuo ili kujihakikishia namna ya kuishi baada ya kufukuzwa kazi. Hatimae tajiri wake alimwona ni karani mwenye busara kwa lile alilolifanya.
Wewe JE? Utafanya nini baada ya kuufikia ukomo wako wa kuwepo shuleni / kazini? Utafanya nini, ukifukuzwa kazi unayoifanya sasa? Utafanya nini mwili wako utakapokuwa hawezi? Utakuwa nani /utaishi na nani/ utaonekanaje baada ya nafasi uliyonayo kufika tamati? Utakuwa mgeni wa NANI
Unapaswa kuwa na majibu ya maswali hayo mapema kabla haujafika ukomo wa wakati wako uliokubalika. Anza kufanya maandalizi ya kuondoka mahala uliposimama leo wakati bado unayo nafasi ya kutosha, unazonguvu za kutosha, kabla haujaja wakati wa kuondoka kwa LAZIMA!