Jikumbatie
Jikumbatie
Tunaishi kwenye jamii ambayo watu wengi wamekata tamaa au wamekatishwa tamaa. Jamii yen ye watu wen ye chuki na wivu uliopitiliza. Mtu yupo tayari kutumia nguvu zake kuhakikisha mwingine hapati fursa fulani. Jamii isiyokubali kabisa mafanikio. Mtu akipata mafanikio anakuwa adui.
Hii ndio aina ya jamii ambamo tunaishi.Jamii inayotaka kusikia anguko la watu. Kusikia fulani ametenguliwa kwenye nafasi aliyokuwepo. Kusikia mtu amesimamishwa kazi au ameshushwa cheo. Kusikia mtu ameachana na mume au mke wake. Hizi ndizo taarifa ambazo hupokelewa kwa mikono miwili. Kama unabisha fuatilia kwenye mitandao ya kijamii kama hutayaona haya waziwazi. Pamoja na yote haya, unawezaje kuishi kwenye jamii hii na ukabaki salama? Ukaepukana na hiki ambacho siku hizi tunakiita 'changamoto ya afya ya akili'? Mimi nakuambia jikumbatie. Jikumbatie katika hali yoyote ambayo unapitia. Wewe ndio kitu pekee cha uhakika katika maisha yako. Marafiki wanaweza kuondoka, mpenzi halikadhalika. Isivyo bahati wewe huwezi kuondoka ukajiacha.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza