Your Basket

Checkout | Shopping Cart
Kibaruani - GetValue
Biashara & Ujasilimia Mali

KIBARUANI

0
0
  • 5
  • 4
  • 3
  • 2
  • 1
Price:
10,000 Tsh.
Added To Cart:
0
Added to shop:
Dec 25, 2025
Product Views:
21
In category:
Sample

USIYOYAFAHAMU KUHUSU ENEO LAKO LA KAZI

NIAMBIE: NINI KINAENDELEA KIBARUANI KWAKO? KIBARUANI ni eneo lako na langu la kazi; mfanyakazi wa ofisini, kwenye taasisi, kiwandani, super market, machimboni, sokoni, bodaboda na kokote ambako unafanya shughuli zako au kutoa huduma ili kujipatia riziki. Lakini pia naweza kusema Kibaruani ni sehemu ambapo watu wanakusanya nguvu, maarifa na weledi wao kutengeneza faida au wakati mwingine kutengeneza hasara. Kibaruani ni sehemu ya fursa ambayo watu kwa nyakati tofauti tofauti wanaingia kwa kuajiriwa na kutoka pale ajira zao zinapokoma au kukamilika kwa huduma wanayoitoa. Ni sehemu ya fursa kwa sababu watu hutumia nguvu, akili, maarifa na ubunifu wao kuzalisha na hivyo kujipatia kipato na wakati huo huo kutengeneza faida kwa taasisi, kampuni au waajiri wao. Ni sehemu ya ukuaji kifikra na kujitambua, ni sehemu ya kuwa mtu fulani au kutimiza ndoto fulani kubwa na ni sehemu inayokupa fursa ya kuonyesha ulichonacho na kikaonekana. Kwa sababu hii Kibaruani ni sehemu ambayo huwavutia wengi; watalamu, vijana waliohitimu vyuoni na wale ambao hawakubahatika kupata elimu ila wana maarifa ama nguvu ya kuweza kuzalisha na hivyo kuwa sehemu ya walio Kibaruani. Tunasomesha au kuandaa vijana wetu kuja kuwa watu sahihi wa Kibaruani, watu ambao watatumainiwa kwenye mnyororo wa uzalishaji na hata tunaowaandaa kujiajiri mwisho wa siku tunatamani wawe pia waajiri. Lakini kwa jicho lingine, Kibaruani ni sehemu ya changamoto ambazo wakati mwingine zinatukimbiza baadhi yetu kwa kupaona Kibaruani pachungu, changamoto zinazodidimiza ndoto zetu na ambazo wakati mwengine zinagharimu ubinadamu wetu, utu wetu na mustakabali wa maisha yetu kwa ujumla. Changamoto ninazozizungumzia hapa ni zile ambazo sio fursa kwa kibarua kwa ujumla wake. Changamoto hizi kwa kiasi kikubwa ndio zinafanya tuondoke maeneo ambayo awali tuliamini ni maeneo ya ndoto zetu, sehemu ambazo tulidhani zingebadili maisha yetu, sisi na familia zetu, sehemu ambazo tuliamini vipaji vyetu na mchango wetu ungeonekana na kuzalisha faida. Na kwa kweli changamoto hizi ambazo kwa sehemu kubwa kitabu hiki kinaziangalia, hazikosekani Kibaruani. Ni pete na kidole katika maeneo yetu tunakofanya kibarua. Kitabu hiki hakitoi majibu au suluhisho la moja kwa moja ya yale yanayoendelea maeneo ya kazi kwa maana ya changamoto bali kinajaribu kuziongelea na kuziweka wazi. Bila shaka wewe msomaji wangu ungetamani kuzifahamu na pengine umekuwa ukizipitia, na kama si wewe pengine ni mtu wako wa karibu na unatamani matendo haya yasiwe sehemu ya Kibaruani kwako na kwangu ili kupafanya Kibaruani kwa asilimia kubwa pawe sehemu ya fursa na furaha muda wote na kwa asilimia chache sana, pawe sehemu ya changamoto.

More Products On Discount
Best Sellers List
Best Seller
1,000 Tsh.
(5.4)

Sold by: Gaston Ngailo

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PASTOR TONY OSBORN

Best Seller
10,000 Tsh.
(69.8)

Sold by: Samuel Macha

Best Seller
3,000 Tsh.
(16.4)

Sold by: ABDULKADIR MASSA

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PETER TARIMO

Best Seller
150,000 Tsh.
(3.6)

Sold by: Gaston Ngailo

GetValue Recommendations
Old is Gold