Your Basket

Checkout | Shopping Cart
Nafsi Iliyonisaliti - GetValue
Biashara & Ujasilimia Mali

NAFSI ILIYONISALITI

0
2
  • 5
  • 4
  • 3
  • 2
  • 1
Price:
10,000 Tsh.
Added To Cart:
0
Added to shop:
Dec 20, 2023
Product Views:
368
In category:
Sample

Mwili, ndoa, watoto, utajiri, imani, dhambi, hukumu na toba ni matukio ambayo aghalabu mwanadamu hana budi kuyapitia katika maisha yake tangu kuzaliwa hadi kutoweka duniani. Makwazo, shida, misukosuko, kukata tamaa, kujisikia kufakufa na mateso ya magonjwa hutokana na tabia za mwanadamu katika mienendo yake katika mambo hayo. Kwa upande mwingine, furaha, mafanikio katika maisha, amani na kukua kwa imani ya kweli katika matendo kadhalika hutegemea mambo hayo manane. Heri mtu yule ambaye matokeo ya mambo hayo humpa furaha na matumaini ya kuingia katika Yerusalemu mpya. rnPole na ole kwa msomaji ambaye matokeo yake humkosesha raha, furaha na matumaini ya kuishi. rn‘’Nafsi Iliyonisaliti’’ ni kitabu kinachokuonyesha jinsi ambavyo nafsi ya mtu inavyoweza kumtia najisi na kumtesa kiasi cha kukosa imani, tumaini la kuishi maisha ya raha, amani na upendo na mwisho kupoteza uhai. Matatizo yatokanayo na mambo hayo ni mengi na makubwa: rn• Ndoa kukosa amani, kufarakana na kutengana. rn• Watoto kuhangaika mitaani kwa kukosa malezi bora baada ya ndoa za wazazi wao kuvunjika.rn• Kiu ya utajiri wa haraka na kutaka mali sababu ambazo kwa kiwango kikubwa hugharimu maisha ya vijana wengi kutamani kujiunga kwenye imani zisizoeleweka na kufunga maagano katika ulimwengu wa giza ambayo huwafanya kuwa watumwa wa dhambi. rn• Vifo kuongezeka.rn• Kuporomoka kwa maadili mema katika familia na jamii.rn• Kupotea imani ya kweli katika matendo.rn• Kupungua na kutoweka kabisa hofu ya Mungu.rnrnMshahara wa dhambi ni mauti. Hukumu ya dhambi ni kifo. Hukumu imekwisha kutolewa kwa ye yote atendaye dhambi asipogeuka, kuomba toba ya kweli iletayo wokovu katika Yesu Kristo, yaani upendo, imani ya kweli na tumaini jipya.rnrnDunia imebadilika, maadili hakuna tena, matukio ya hatari na kutisha yamegharimu maisha ya mamia na maelfu ya watu duniani kwa sababu ya dhambi. Matetemeko ya ardhi, vimbunga, vyombo vya majini kuzama na ndege kutoweka angani ni baadhi ya matukio ambayo hayawezi kusahaulika katika historia ya ulimwengu. Dalili za siku za mwisho, gharika jipya kutokea, angamizo jingine mfano wa Sodoma na Gomora zaonekana bayana. “Sisi je tutapataje kupona tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia.” (Waebrania 2:3).rnKwa nini kuendelea kuteseka? Kwa nini kuendelea kumtumikia Ibilisi? Kwa nini kuchagua kuziacha njia za kweli kwa kuzifuata njia za maumivu, mateso, karaha na mauti zisababishazo kifo? Majibu ya maswali haya na suluhisho la matatizo yaliyopo yanaweza kupatikana katika nafsi, akili na mawazo. Tafuta chanzo cha shida zilizopo kuweza kuzitambua njia ziletayo wokovu. Geuka, badilika, kubali kutubu, kutii na kuokoka upate kuishi maisha mapya katika upendo na kumtegemea Kristo Yesu kama Mlinzi, Mwokozi, Mkombozi na Bwana wa maisha yaliyopo sasa na yatakayo kuwapo baadae. Mungu, Baba, aliyemtuma Kristo Yesu ili kuwakomboa wenye dhambi aongoza na kuonyesha njia za kutokea hata kuufikilia ushindi katika mambo yote.rnrnMsaada wa Mungu ni muhimu sana po pote kitakaposomwa kitabu hiki. Fuatana na mwandishi Jones M. Rugakingira, Sura kwa Sura ili kuweza kuyaona maisha halisi katika nuru ya Kristo. Mungu akubariki. Amina.

“Mwenye kuchimba shimo hutumbukia ndani yake; Na yeye abomoaye boma, nyoka atamwuma. Mwenye kuchonga mawe huumizwa kwayo; Naye apasuaye miti huona hatari katika hiyo. Iwapo chuma hakipati, wala mtu hakinoi; Ndipo hana budi kutumia nguvu zaidi. Walakini yafaa kutumia hekima, na kufanikiwa… Maneno ya kinywa chake mwenye hekima yana neema; Bali midomo ya mpumbavu itammeza nafsi yake. Mwanzo wa maneno ya kinywa chake huwa ni upuuzi; na mwisho wa usemi wake ni wazimu wenye hatari.” (Mhubiri 10: 8-10, 12-13).rn
rnMawingu yakiwa yamejaa mvua, Yataimimina juu ya nchi; Na mti ukianguka kuelekea kusini, au kaskazini, Paangukapo ule mti, papo hapo utalala… Kama vile wewe usipoijua njia ya upepo ni ipi, wala jinsi mifupa ikuavyo tumboni mwake mjamzito; kadhalika huijui kazi ya Mungu, afanyaye mambo yote. Asubuhi panda mbegu zako, Wala jioni usiuzuie mkono wako. Kwa maana wewe hujui ni zipi zitakazofanikiwa, kama ni hii au hii, au kama zote zitafaa sawasawa.” (Mhubiri 11: 3, 5-6).rn
rn“Nafsi Iliyonisaliti” ni miongoni mwa vitabu vilivyo tayarishwa na Jones M. Rugakingira. Baada ya kuandika kwa mafanikio ya kiroho vitabu viwili “Kushinda Nguvu ya Dhambi” na “Nguvu ya Imani” sasa anakuletea kitabu hiki ili kukusaidia kukikuza kiwango cha imani. Kuteleza si kuanguka. Kuvunjika kwa koleo siyo mwisho wa uhunzi. Maisha ya sasa ni matokeo ya matendo katika imani nyakati zilizopita. Maamuzi ya sasa ni matokeo ya maisha ya kesho. Amua vema sasa upate maisha mema siku zinazokuja.rn
rnFuatana na Mwandishi Jones M. Rugakingira ili kujifunza mengi yanaweza kuchangia kukufikisha mahali ulipo sasa. Roho Mtakatifu akuongoze katika usomaji. Wema wa Mungu watosha.rnrn

More Products On Discount
10,000 Tsh. 7,000 Tsh.

Sold by: Godius Rweyongeza

7,000 Tsh. 2,999 Tsh.

Sold by: Said Maumba

6,000 Tsh. 5,000 Tsh.

Sold by: Godius Rweyongeza

10,000 Tsh. 7,000 Tsh.

Sold by: Godius Rweyongeza

10,000 Tsh. 9,000 Tsh.

Sold by: Godius Rweyongeza

Best Sellers List
Best Seller
1,000 Tsh.
(5.4)

Sold by: Gaston Ngailo

Best Seller
10,000 Tsh.
(69.8)

Sold by: Samuel Macha

Best Seller
3,000 Tsh.
(16.4)

Sold by: ABDULKADIR MASSA

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PETER TARIMO

Best Seller
4,000 Tsh.

Sold by: Mashaka Khamis

GetValue Recommendations
5,000 Tsh.

Sold by: Denis Mpagaze

10,000 Tsh.
(1)

Sold by: PJ PROJECTS

12,000 Tsh.

Sold by: Germano Mbelwa

5,000 Tsh.

Sold by: Sabas Patrick

25,000 Tsh.

Sold by: PJ PROJECTS

Old is Gold
1,000 Tsh.

Sold by: Jabir Khamis

4,000 Tsh.

Sold by: Said Maumba

10,000 Tsh.

Sold by: Joseph Hoja