NAMNA YA KUWAVUTIA WATEJA KWA KUTENGENEZA THAMANI YA MTEJA
Sanaa ya kuwavutia wateja kwenye biashara yako si uchawi bali inategemea sanaa ya \"kuunda/kutengeneza thamani ya mteja\" na\r\nuwasilishaji wa pendekezo lake kwa wateja husika.
Lengo la kitabu hiki ni kujadili michakato muhimu ya jinsi mtu anavyoweza kuwavutia wateja wengi zaidi kwenye biashara yake kupitia uundaji au utengenezaji wa thamani ya mteja na uwasilishaji wa pendekezo lake kwa wateja husika na kwa wakati unaofaa. Majadiliano katika kitabu hiki yamewasilishwa katika sura tano kama ifuatavyo:(i) Sura ya Kwanza: Inafafanua neno Mteja, inajadili kategoria tofauti za wateja na jinsi ya kuzishughulikia; (ii) Sura ya Pili: Inafafanua maneno “Tabia ya Mteja” na kujadili hali zinazoathiri tabia ya mteja kwa wakati fulani; (iii)Sura ya Tatu: Inafafanua maneno “Thamani ya Mteja” na kujadili jinsi ya kuiunda/kuitengeneza kwa bidhaa na huduma; (iv) Sura ya Nne: Inafafanua\\r\\nmaneno “pendekezo la thamani ya Mteja”, inajadili uundaji wake, uwasilishaji, na umuhimu wake kwa huluki ya biashara, na (v) Sura ya Tano: Inajadili umuhimu wa “Uundaji wa Thamani ya Mteja” kama inavyotumika katika Dhana ya Kujiajiri. Kitabu hiki kinafaa kwa wajasiriamali wapya, wanafunzi wa shule za biashara na vyuo vikuu, watu wanaopanga kujiajiri, wakufunzi wa ujasiriamali na wasomaji wowote wanaotaka kulinganisha maelezo katika uwanja wa mvuto wa wateja. Msomaji anaweza asiwe mtaalamu wa usimamizi wa biashara isipokuwa awe na shauku katika fasihi ya biashara.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza