NDOA BORA YENYE UPAKO AMANI NA UPENDO WA KWELI
Ni wakati wa ndoa yako, kuwa ndoa Bora yenye Upako, Amani na upendo wa kweli.
Ni mapenzi ya Mungu uwe na ndoa Bora ya kuigwa.
Ndoa Bora ya kuigwa ni ndoa yenye Upako Amani na upendo wa kweli. Ndoa nyingi zimekuwa hazina Upako Amani na upendo wa kweli hivyo kukosa sifa ya kuwa ndoa Bora za kuigwa Kwa sababu wanandoa wengi hawana maarifa sahihi ya Ki-ungu kuhusu ndoa.
Mungu ndio mwanzilishi wa ndoa, kwa hiyo mtu yeyote anayetaka kuwa na ndoa Bora ya kuigwa, sharti awe na taarifa (maarifa) za kutosha kuhusu ndoa ambazo Mungu ametupa pitia neno lake.
Katika kitabu hiki Mch Jackson na mke wake wanafunua kweli ya Mungu itayokupa maarifa sahihi ya Ki-ungu kuhusu ndoa, ambayo ni ufunguo wa kukuwezesha, kuwa na ndoa Bora ya kuigwa.