NJIA 10 ZA KIBIBLIA ZA KUKUSAIDIA KUMJUA NA KUMPATA MWENZA WA MAISHA
Kitabu hiki kitakuongezea ufahamu na maarifa kuhusu njia za kibiblia za kukusaidia kumpata mwenza wa maisha kwa kuwa mke au mume mwenye busara mtu hupewa na BWANA (Mithali 19:14). Mungu hutumia njia mbalimbali kusema na wanadamu juu ya masuala mbalimbali na hivyo mwandishi ameandika njia hizo akifafanua kwa muktadha wa kukusaidia kumpata mwenza wa maisha.
Mwandishi aliandika kitabu hiki kwa mara ya kwanza mwaka 2006 ambapo alisitisha uzalishaji wake mwaka 2010. Sasa, kufuatia mahitaji ya watu na umuhimu wa kitabu hiki kwa vijana wa kiume na wa kike, mwandishi ameona vema kukichapisha tena ambapo amefanya maboresho kadhaa ya kiuandishi, mtiririko wa mawazo na fafanuzi ili kuongeza ubora na upana wa maarifa kwa msomaji. Ndani ya kitabu hiki utajifunza misingi 7 na njia 10 za Kibiblia za kukusaidia kumjua na kumpata mwenza wa maisha.
Karibu ununue kitabu hiki kwa kubonyeza sehemu ya ‘Buy now’ ili ujipatie ufahamu na maarifa husika. Pia kwa kufanya hivyo utakuwa umechangia kazi ya uandishi wa vitabu vingine ambavyo Patrick Sanga anaendelea kuviandika. Licha ya uandishi wa vitabu, Patrick Sanga ni mwandishi wa masomo ya neno la Mungu na mengine mahususi kuhusu Roho Mtakatifu, vijana, wanawake, ndoa na siku za mwisho nk. Ikiwa utapenda kusoma masomo hayo, tafadhali tembelea blogu za www.sanga.wordpress.com na www.sanga.co.tz
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza