USICHOKIJUA KUHUSU MALEZI
Miongoni mwa mambo yanayojenga ama kubomoa hatima ya mtu ni sauti za ndani, vifungo hisia, tafsiri isiyo sahihi kuhusu upendo, kunyanyaswa na kudekezwa. Bahati mbaya yote haya ni matokeo ya namna mtoto anavyolelewa. Kwa wazazi wengi, watoto huaribiwa na mazingira, marafiki na utandawazi lakini mantiki ya malezi ni uwepo wa mtu kwenye maisha ya mtoto ambaye atamsaidia kutoathiriwa na hivi vyote. Ikiwa hivi vimefanikiwa kumuharibu mtoto, tatizo ni la mzazi. Kitabu hiki kina mbinu, maarifa na majibu ya maswali yako mengi kuhusu malezi salama ya watoto wako ikiwa unatamani awe na hatima njema. Kukisoma na kuyafanyia kazi kuna faida kubwa kuliko matunzo mazuri unayompatia mtoto.
Kitabu bora cha Malezi ambacho
1. Kinamsaidia msomaji kuona jinsi alivyolelewa na namna malezi yamemfanya kuwa alivyo
2.Mzazi kujitathmini anamlea vipi mtoto wake na itamfanya mtoto wake aweje
3. Mbinu za kumlea mtoto ili afikie hatima yake
Kimeandikwa na Deogratius Sukambi