Your Basket

Checkout | Shopping Cart
Uwezo Wa Kuanzisha Na Kukuza Biashara - GetValue
Biashara & Ujasilimia Mali

UWEZO WA KUANZISHA NA KUKUZA BIASHARA

0
0
  • 5
  • 4
  • 3
  • 2
  • 1
Price:
10,000 Tsh.
Vendor:
Added To Cart:
0
Added to shop:
Aug 28, 2023
Product Views:
574
In category:
Sample

Amsha Nguvu Iliyolala Ndani Yako Kujenga Biashara Yenye Mafanikio

Na mimi naweza kuwa na biashara? Kuna biashara inayoweza kukupa faida? Nifanye biashara gani? Na mimi naweza kuwa tajiri? Haya ni baadhi ya maswali ambayo yamekuwa yakijirudia sana vichwani mwa watu. Haya ni maswali ambayo watu huwa wanajiuliza pale wanapofikiria kuhusu biashara kama njia ya kuingiza kipato.

Baada ya kuziona biashara nyingi zikianzishwa kisha kufa baada ya muda mfupi, hofu hutanda kwa watu kama kuna uwezekano wa kukuza biashara na kufikia mafanikio makubwa. Pia baada ya aina nyingi za biashara kuonekana kuanzishwa, watu hufikiri hakuna biashara nyingine ambazo wao wanaweza kuzifanya, wakiamini mawazo yote yameshachukuliwa. Dhana hii huwaaminisha kuwa hakuna wazo jipya la biashara la wao kufanyia kazi.

Je ni kweli huna uwezo wa kuanzisha na kukuza biashara na kuifikisha kwenye mafanikio makubwa? Jibu ni hapana. Matatizo mengi ya kutoanzisha au kutoweza kukuza biashara baada ya kuianzisha yanaanzia kwenye mtazamo. Mtazamo ni mawazo yenye imani yanayoamua hatua za kuchukua. Moja ya nguvu ambayo unayo ndani yako unayoweza kuiamsha na kufanya mapinduzi makubwa maishani mwako ni fikra (mtazamo).

Biashara ni za watu fulani maalumu, kabila fulani maalumu, watu wenye mitaji fulani. Mimi sina uwezo wa kufanya biashara. Hizi

ni dhana pia zilizojengeka kwa watu na kuwazuia hata kuanzisha biashara au hata wakianzisha kutoweza kuzikuza. Hiki pia ni kikwazo cha mtazamo ambacho kimewakwamisha watu wengi kuanzisha biashara. Kila mtu ni maalumu, ana uwezo maalumu wa kuanzisha biashara maalumu.

Sina mtaji. Hili ni neno ambalo linasikiwa kwa watu wengi wakieleza kwa nini hawawezi kuanzisha biashara. Lakini ukifanikiwa kujenga ufahamu sahihi na hamasa, hii haitakiwi kuwa sababu ya kwa nini usianzishe biashara. Kuna biashara ambazo unaweza kuanza hata bila ya mtaji. Kuna vitu unavimiliki sasa vinavyoweza kukupa mtaji. Lakini kama una kipato kidogo unaweza kuweka akiba mpaka unapata kiasi cha kuwa mtaji.

Wapo watu waliopo kwenye ajira na kuona ajira zao ni kikwazo cha wao kutokuwa na biashara. Wapo walioanzsisha biashara kwenye ajira lakini wameishia kupoteza mitaji yao. Je ni kweli huwezi kuianzisha na kuikuza biashara ukiwa kwenye ajira? Jibu ni hapana, kuna uwezekano huo. Kitabu hiki kinaenda kukueleza kwa kina namna ya kuanzisha na kuikuza biashara yako ukiwa kwenye ajira.

Biashara hazidumu zinakufa. Hiki ni kilio cha watu wengi. Kuna taarifa mbaya kuhusu biashara; 90% ya biashara zinazoazishwa zinakufa ndani ya miaka 5 huku 80% zikiwa zinakufa ndani ya miaka 2. Hii si habari nzuri kuisikia, lakini inakuonyesha changamoto iliyopo kwenye kufanya biashara.

Taarifa hizo hapo juu zinaonyesha kuna kitu kinachokosekana kwenye biashara kikisababisha biashara nyingi kufa baada ya muda mfupi tangu kuanzishwa. Lakini kama kuna biashara zinazokuzwa na kufikia mafaniko makubwa, ina maana kuna vitu ambavyo wale waliofanikiwa kwenye biashara wanafanya wakati walioshindwa hawafanyi. Kitabu hiki kitaelezea siri hiyo kisha na wewe kuitumia na kufanikiwa kuikuza biashara yako.

Kama nyumba huhitaji kujengwa kwenye msingi imara ili kuweza kudumu hata dhoruba zikija, vivo hivyo unahitajika kujenga biashara yako kwenye misingi imara, ili iweze kuimarika na kusimama wakati wa dhoruba. Kitabu hiki kinaeleza misingi hiyo, ambapo ukianzakuijenga, hakika biashara yako haitaanguka itakapokuwa inakutana na changamoto mbalimbali.

Tangu umezaliwa unashuhudia jua likichomoza na kuzama kila siku bila ya kushindwa wala kuahirisha. Kunakuwa na kitu kinachowezesha zoezi hili kufanyika kwa ufanisi mkubwa, kiasi hicho na kutoshindwa. Ndiyo, kitu hicho kipo, nacho ni mfumo unaohakikisha kila sukunde dunia inaendelea kuzunguka kwenye mhimili wake kwa ufanisi mkubwa. Biashara nazo ili ziweze kujiendesha zenyewe na kwa ufanisi mkubwa, unahitaji kuitengenezea mfumo tangu mwanzo. Hiki ni kitu kilichokosekana kwenye biashara nyingi na kupelekea biashara hizo kutetereka na hata kufa. Kitabu hiki kitakusaidia kukuelekeza namna ya kujenga mfumo wa biashara ili iweze kujiendesha yenyewe hata kama wewe hupo.

Moyo wa binadamu ukiacha kudunda, uhai wake unaishia pale. Hivyo ili viungo vingine viendelee kufanya kazi vinahitaji moyo uendelee kudunda. Biashara nayo ina moyo, moyo wake ni mauzo. Bila mauzo hakuna biashara, mauzo yakisimama, biashara inasimama. Hivyo lazima kuwe na mikakati madhubuti kuhakikisha biashara inaendelea kuuza. Hili ni eneo ambalo kitabu hiki limekipa uzito unaostahili ili biashara yako utakayoianzisha iendelee kudunda huku ikikua.

Kipato duni na utumwa wa kifedha ni kilio cha watu wengi. Licha ya jitihada nyingi zinazowekwa ili kupata kipato, lakini kimekuwa hakitoshi. Hata fedha za kukidhi mahitaji ya kawaida imekuwa changamoto kwa watu wengi. Lakini watu wengi pia wameishia kuishi maisha yaliyopo na siyo wanayostahili kwa sababu ya fedha. Kipato cha uhakika kitatoka wapi? Je ni kuajiriwa au kujiajiri? Jibu ni hapana. Utajiri wa kukupa uhuru wa kifedha upo kwenye kujenga biashara yenye mafaniko. Moja ya dhumuni la kitabu hiki ni kukuwezesha kuwa na na kipato cha kutosha kwa wewe kuweza kujenga biashara yenye mafanikio makubwa.

Je wajua kuwa tayari una mtaji wa awali kuanzisha biashara yenye mafanikio makubwa? Una mtaji ndani yako ambao ni uwezo wa kukuwezesha kufanya biashara kwa mafanikio makubwa. Tafiti zinaonyesha kuwa licha ya dunia kupata mafanikio makubwa kiasi hiki, binadamu ametumia wastani wa 10% ya uwezo wake. Hivyo ndani yako kuna nguvu kubwailiyolala tu ambayo unaweza kuiamsha na kutumia kuanzisha na kukuza biashara. Kwa sababu nguvu hiyo tayari ipo ndani yako, kilichobaki ni kuwa na mikakati ya kuiamsha ili ikunufaishe. Kitabu hiki kitakupa mikakati hiyo ya kunufaika na hazina hiyo kupitia biashara.

Licha ya biashara kuwa na fursa ya kukua kwa haraka na kukupa kipato kikubwa, lakini ina hatari kubwa sana ya kutetereka na kufa inapokutana na changamoto mbalimbali. Hivyo kuendelea kutengeneza fedha au utajiri bila ya kuwa na mkakati wa kuzitunza ni kujiweka kwenye hatari kubwa ya kupoteza kile unachoweza kuwa umekitafuta kwa muda mrefu. Njia kuu ya kuulinda utajiri wako ni kuwekeza maeneo sahihi. Hili ni lengo mojawapo la kitabu hiki, kuhakikisha unatunza utajiri wako utakaokuwa umeutolea jasho.

Ndugu! Wewe ni miongoni mwa watu wenye uwezo wa kuanzisha biashara kuanzia chini kabisa, kuikuza na kuifikisha kwenye mafanikio makubwa. Inawezekana kuanzisha biashara limekuwa wazo lako la siku nyingi sana ambalo halitekelezeki. Umejiuliza wapi nitaanzia lakini umekosa majibu. Umeziona biashara nyingi zikifa, na zikakutia hofu. Basi wakati sahihi wa kuanza na kukuza biashara yako umefika.

Kwa sababu nguvu ya kuanzisha na kukuza biashara tayari ipo ndani yako hivyo kilichobaki ni mwongozo na utayari wa kuamsha nguvu hiyo ili uweze kujenga biashara ya mafanikio ya ndoto yako. Hili ndilo dhumuni kuu la kitabu hiki kukuwezesha kuamsha nguvu kubwa uliyonayo kufanya makubwa katika maisha yako kupitia biashara.

Mpaka unamaliza kusoma kitabu hiki unatarajiwa uwe umepata wazo la biashara na kuianzisha. Na kama tayari ulikuwa na biashara unatarajiwa uwe umeshapata mikakati thabiti ya kwenda kuikuza biashara yako na kufikia mafanikio makubwa. Karibu sana na nakutakia usomaji mwema.

Ndugu yako katika mafanikio, Alfred Mwanyika.

More Products On Discount
10,000 Tsh. 7,000 Tsh.

Sold by: Godius Rweyongeza

3,999 Tsh. 1,999 Tsh.

Sold by: Daudi Lubeleje

9,000 Tsh. 7,500 Tsh.

Sold by: MTALIMBO BOOKS

6,000 Tsh. 5,000 Tsh.

Sold by: Godius Rweyongeza

Best Sellers List
Best Seller
2,000 Tsh.
(5.4)

Sold by: Gaston Ngailo

Best Seller
10,000 Tsh.
(69.8)

Sold by: Samuel Macha

Best Seller
3,000 Tsh.
(16.4)

Sold by: ABDULKADIR MASSA

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PETER TARIMO

Best Seller
4,000 Tsh.

Sold by: Mashaka Khamis

GetValue Recommendations
5,000 Tsh.

Sold by: Denis Mpagaze

10,000 Tsh.
(1)

Sold by: PJ PROJECTS

12,000 Tsh.

Sold by: Germano Mbelwa

5,000 Tsh.

Sold by: Sabas Patrick

25,000 Tsh.

Sold by: PJ PROJECTS

Old is Gold