
UZURI WA GEREZA Hazina Iliyo Sahaulika
UZURI WA GEREZA Hazina Iliyosahaulika sehemu ya 2
Sehemu Ya Pili
Gerezani Ni Mahali Ambapo Watu Wenye Tabia Na Hulka Mbaya Wanalazimishwa Kukaa Kinyume Na Matakwa Yao Bali Wanakalishwa Humo Kwa Mujibu Wa Sheria, Kazi Kubwa Ya Gereza Ni Kuwahifadhi Watuhumiwa Ambao Mashauri Yao Hayajatolewa Maamuzi Mahakamani (Mahabusu). Linawahifadhi Watu Waliopatikana Na Hatia Kisha Kupewa Adhabu Za Vifungo Vya Muda Maalum. Vifungo Vya Maisha Kwa Ajili Ya Urekebu Wa Tabia (Wafungwa) Na Waliopatikana Na Hatia Kisha Kupewa Adhabu Ya Kunyongwa Hadi Kufa Kwa Wanawake Na Wanaume Wakiwa Wametenganishwa Kijinsia (Kondemu). Gerezani Kuna Baadhi Ya Mambo Ambayo Siyo Mazuri Na Baadhi Ambayo Ni Hazina Ya Thamani Sana Iliyosahaulika Yanayoweza Kuleta Mapinduzi Makubwa Ya Kiroho, Kijamii, Kiutamaduni, Kiuchumi Na Kiujasiriamali Katika Taifa La Tanzania Na Kuwa Chachu Ya Mapinduzi Kwa Bara Zima La Afrika Kutoka Ndani Ya Magereza Ya Tanzania. Kitabu Hiki Ni Taarifa Rasmi Na Maalum Kwa Ajili Ya Kuondoa Ajenda Za Kishetani Kwa Mtu Binafsi Na Kwa Taifa Zinazostawishwa Na Athari Mbaya Za Utandawazi Ili Kujenga Utandawazi Wa Maendeleo Endelevu Ya Kiroho Kwa Ajili Ya Kujitawala Kifikra Na Kuutawala Ulimwengu Unaolizunguka Taifa La Tanzania. Usipange Kutokukisoma Kitabu Hiki, Kwani Ni Ufunguo Wa Kufungulia Mlango Wa Hatima Njema Kuhusiana Na Maisha Yako Binafsi, Na Hatima Njema Ya Taifa La Tanzania Na Bara Zima La Afrika.