
MAOMBI YALETAYO MAJIBU
Price:
8,000 Tsh.
Vendor:
Added To Cart:
0
Added to shop:
Mar 16, 2023
Product Views:
135
Sample
Watu wengi wamekuwa wakiomba mahitaji yao kwa Mungu na kujibiwa kama walivyoomba, lakini unakuta katika maisha yao binafsi kuna shida mbalimbali\r\nzinazowafanya\r\nwashindwe kutumia vitu walivyoviomba kwa furaha, uhuru na amani. rnrnNdio maana neno la Mungu likasema katika kitabu cha Waebrania 12:14, “Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;”
MAOMBI YALETAYO MAJIBU ni kitabu kilichobeba mambo makubwa sana na ya msingi yawezayo kukusaidia kubadilika katika kuomba kwako na hatimaye kufikia lengo lililokusudiwa katika kuomba kwako.
Asilimia kubwa ya wakristo huomba bila kupata matokeo chanya katika maombi yao. Na hilo hutokea kwa sababu tofauti tofauti kama vile kutokujua waombaje ili wapate majibu, kushindwa kufuata hatua za muhimu sana katika maombi, na kadhalika.
Nataka nikueleze kwamba, Mungu wetu huwa anajibu maombi tunayomuomba, na wakati mwingine zaidi ya hayo tunayomuomba sawasawa na mapenzi yake.
Kukosa ufahamu na maarifa ya kutosha juu ya namna Mungu anavyojibu maombi imekuwa sababu mojawapo ya kuendelea kuomba bila kupokea majibu.