VITA MALANGONI
VITA MALANGONI (Vita inayoinuka katika malango dhidi ya baraka zako, familia na hatima yako na jinsi ya kuishinda)
Anza kwa kujiuliza maswali haya katika maisha yako;
Kwanini kila mara unapokaribia hatua kubwa katika maisha, mambo huwa magumu zaidi? unapokaribia kupata ajira, ndoa, kuhitimu, kupata tenda kubwa au kupokea baraka kubwa ambayo uliisubiri kwa muda mrefu ndipo changamoto kubwa zaidi huinuka?
Kwa nini vita vya kiroho na vikwazo huongezeka unapokaribia mafanikio?
Jibu ni moja: unakuwa kwenye lango au unakaribia lango la baraka husika na kila lango lina vita.
Katika ulimwengu wa roho, \"Malango\" ni maeneo ya mpito, ya kiingilio, au ya maamuzi yanayofungua njia ya vitu kupita kuingia kwenye hatima ya mtu, maeneo haya hushambuliwa zaidi ili kuzuia baraka kupita. Ndiyo maana kuna watu wanasali sana, wana bidii sana lakini kila wanapokaribia kufanikiwa mlango wa mabadiliko huwekewa zuio, Hapo ndipo hufanyika “vita malangoni.” Vita ya malangoni ni halisi, ni vita inayoleta uharibifu, ucheleweshwaji, zuio la baraka za Mungu.
Kitabu hiki ni mwongozo wa ufunuo wa kiroho utajifunza; Dhana ya vita malangoni, aina za malango, Kwanini adui anapigana na mbinu anazotumia kushambulia malango yaliyobeba baraka zako. Mbinu na silaha za kimkakati zitakazokusaidia kufungua na kumiliki malango ya baraka zako.
Malango yako yanahitaji kulindwa. Huu ni ufunuo wa wakati, kwasababu pamoja na vita ushindi upo na unawezekana, kwa sababu tunaye Mungu: “…Na milango la kuzimu haitalishinda...” (Mathayo 16:18)
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza