VYANZO 10 VYA FURAHA
VYANZO 10 VYA FURAHA
Kwa kawaida binadamu hupitia changamoto mbalimbali kwa wakati tofauti tofauti katika maisha yao ikiwemo kukosa kazi, kuanguka kiuchumi, kupigwa, kufokewa, kutukanwa, kupelekeshwa, kujibiwa vibaya, kubakwa, kubaguliwa, kufukuzwa kazi au kufukuzwa nyumbani na mengine mengi yenye kuleta maudhi ambapo huwa wanabaki wanasumbuliwa kwa kuyakumbuka mambo haya na kupelekea kupata hasira hali hiyo huendelea kuwatesa mpaka wanakosa furaha.
“VYANZO 10 VYA FURAHA” ni kitabu kilichoandika kwa lengo la kuelimisha na kutoa mwongozo kwa kueleza mambo kumi yanayosaidia kuleta furaha kwa watu wanaoishi maisha yasiyo na furaha kwa sababu mbalimbali ambazo walikumbana nazo katika kipindi cha nyuma cha maisha yao au wanakumbana nazo kila uchao na wanashindwa namna ya kurudisha furaha yao hivyo wanabaki kuwa na huzuni na msongo wa mawazo maishani mwao.