WAPINDUA ULIMWENGU
Wapindua Ulimwengu ni zaidi ya kitabu ni wito unaowaita watu wa rika zote bila kuangalia dini, imani, jinsia, taifa, kabila, lugha, umri, cheo au elimu, ili wapate kumwakilisha Mungu katika mifumo mbali iliyoharibika ya ulimwengu.
Tunaishi katika nyakati za mwisho za hatari, nyakati ambazo ulimwengu umechafuka kwa maovu na maasi mengi ya kila namna. Kwa mara nyengine tena Mungu yupo kazini kujiinulia kizazi cha watu muhimu atakaowatumia kwa nguvu katika hizi siku za mwisho kuleta mapinduzi na mageuzi katika sekta mbali mbali kuanzia kiroho, uchumi, biashara, siasa, uongozi nk
Kitabu hiki kitakupa ufahamu mkubwa na ufunuo kuhusu siri za kukuandaa kuwa mtu mkuu, mtu mwenye matokeo, mleta mageuzi na mabadiliko kwa ngazi ya familia, kanisa, jamii, taifa na ulimwengu kwa ujumla.
Baadhi ya mambo utakayojifunza kwenye kitabu hiki ni:
1. Nguvu ya utakatifu katika kukuandaa uwe mtu mkuu.
2. Nguvu ya Roho Mtakatifu katika kukuandaa uwe mtu mkuu.
3. Ngazi 7 za kupanda za Imani ili upate matokeo makubwa.
4. Kushinda roho ya hofu kama kikwazo cha kufikia ukuu wako.
5. Uwekezaji wa kumjua Mungu kibinafsi kama kigezo cha kufikia ukuu.
6. Nafasi ya maombi katika kupindua ulimwengu.
7. Mbinu za kuivamia na kuipindua mifumo ya ulimwengu.
Nipende kukaribisha msomaji wangu kujipatia nakala yako siku ya leo, na uanze safari yako ya mageuzi na mguso katika kizazi chako.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza