• Call us +255 717 568 861

Your Basket

Checkout | Shopping Cart
Ushindi Kimaisha - GetValueInc
Biashara & Ujasilimia Mali

Ushindi Kimaisha

Ratings

Price:
8,000 Tsh.
Vendor:
Num added to cart:
0
Added to shop:
Nov 17, 2020
In category:
Sample

Ushindi Kimaisha Mafanikio Ya Kweli

imepata msukumo wa kuandika kitabu hiki baada ya kusoma vitabu vingi vilivyoandika kuhusu mafanikio mfano kitabu kinachoitwa Siri 200 za mafanikio na maendeleo binafsi (The top 200 secrets of success and the pillars of self mastery kilichoandikwa na Robin S. Sharmd, Siri nane za utajiri wa kweli na jinsi unavyoweza kuzitumia kuboresha maisha yako (8 secret of truly rich people) kilichoandikwa na Mfilipino Bo Sanchez, kitabu cha Inuka, Toka katika Lindi la Umaskini, kilichoandikwa na kijana anayefahamika kwa jina la Joas Yunus Buyungu, Maisha yanayoongozwa na malengo cha Rick Warren na vitabu vingine vingi ambavyo sitaweza kuvitaja hapa. Katika vitabu vyote nilivyosoma vipo ambavyo vimekuwa chachu kwangu na kunitia hamasa ya kuandika kitabu hiki. Mafanikio ya kweli (Ushindi kimaisha) ni hali ya kumjua Mungu wa kweli na kumpa nafasi ya kukutumia apendavyo ili uzae matunda mema kiroho na kimwili. Kila mwanadamu anaweza kuwa na mtazamo wa kwake binafsi juu ya mafanikio lakini ukweli ni kwamba inawezekana akawa na mtazamo mfu. Pia wakati mwingine inawezekana kuwa kuna baadhi ya watu wanaoshindwa kutofautisha kati ya mafanikio ya kweli na utajiri; katika kitabu hiki nimebainisha tofauti zake. Watu wenye mafanikio ya kweli hujitahidi kuweka uwiano kati ya kazi, afya na familia zao. Watu ambao malengo yao ni kupata fedha nyingi huwa na wasiwasi na hushuka moyo kuliko wale ambao wanathamini kuwa na uhusiano mzuri na wengine.

Other products from this category