FAHAMU KUHUSU NDOTO
Price:
15,000 Tsh.
Vendor:
Added To Cart:
0
Added to shop:
Sep 22, 2026
Product Views:
22
Sample
FAHAMU KUHUSU NDOTO (Jinsi ya kuielewa sauti ya Mungu kupitia ndoto unazoota na tafsiri zake kibiblia )
FAHAMU KUHUSU NDOTO
Ni ukweli usiopingika kuwa sote tunahitaji mafanikio na hakuna mafanikio yoyote unayoweza kupata pasipo chanzo na vyanzo huwa ni viwili tu, aidha iwe kwa Mungu au kwa shetani. Chanzo cha kweli ni Mungu na ili ufanikiwe ndani yake lazima uwe na uhusiano naye hakuna namna unaweza kufanikiwa ndani ya Mungu ikiwa hauna mahusiano naye, kama hauwezi kuisikia wala kuielewa sauti yake, ni dhahiri
kuwa hautaweza kufika pale alipo kukusudia uwe, kumbuka uwezo wako wa kuisikia sauti yake utakufanya uelewe na uenende jinsi inavyostahili.
Mungu hutumia njia nyingi sana kuongea na mwanadamu, ikiwamo Neno lake, Watumishi, Maono, Ndoto, Roho Mtakatifu, akiwa na lengo la kuendelea kuweka ukaribu, Changamoto kubwa imekuwa ni kwa mwanadamu kuisikia na kuielewa hiyo sauti, Ni mara chache sana masomo kama haya yamekuwa yakifundishwa, watu wengi wameshindwa kuelewa na kutofautisha sauti ya Mungu na sauti zingine. Kati ya njia nyingi ambazo Mungu amekuwa akitumia kuongea na mwanadamu njia ya ndoto ni mojawapo, Na ni njia kubwa ambayo kila mmoja huweza kuota, ingawa kati ya wengi wanaoota ni wachache wanaoelewa, na kati ya wachache wanaoelewa ni wachache wanaojua cha kufanyaIkulingana na ndoto hizo.Mungu amekuwa akinifunulia mengi kupitia ndoto ambayo mengine yamekuwa ni kwaajili yangu na mengi kwaajili ya wengine pia.
Nimekuwa nikitafutwa na watu wengi sana katika eneo hiliambapo nikaona shida kubwa iliyoko,wengine wamepata hata madhara kupitia ndoto lakini chanzo ikiwa ni
kushindwa kuelewa na kuchanganua ndoto, ndipo Roho Mtakatifu akanipa mwongozo wa kuandika mfululizo wa vitabu kuhusu ndoto ili kuwasaida mataifa yote, kitabu hiki kimechukua miaka kama mitano kuandaa hatua kwa hatua huku nikifunuliwa mambo makubwa na kujengewa uwezo kupitia shuhuda hai za watu, siwezi kusema ni kwa nguvu
zangu ila ni kwa mafunuo kutoka kwa Mungu ili ya kwamba mataifa yaielewe na kuitambua sauti yake na zaidi aendelee kujidhihirisha katika maisha yao na kuwafanikisha.
Katika kitabu hiki utaelewa mambo mengi kuhusu ndoto na utapata mwongozo wa kushughulika na ndoto ili ziweze kuleta athari chanya kama ambavyo Mungu huzitumia. Katika kitabu hiki nimetumia shuhuda hai za watu, nina
shuhuda nyingi mno ambazo ningesema niandike kitabu cha shuhuda tu za watu wanaonifuata basi kingejaa ila katika kitabu hiki nimekuwekea vyote mafunzo na shuhuda ili
uelewe uhalisia wa ndoto na uweze kuvuka.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza