KUOMBA KWA NAMNA AMBAYO UTAJIBIWA
Hata mtu akishindana katika machezo hapewi taji, asiposhindana kwa halali. 2 Tim 2:5
Wengi wanaomba lakini wachache hupata matokeo ya maombi yao. Raha ya maombi ni matokeo/majibu ya maombi yako na sio tu kuomba. Ila kwa bahati mbaya watu wengi hawapati majibu ya maombi yao si kwasababu Mungu hataki kuwajibu ila ni kwa sababu kanuni za kuomba hazikufuatwa. Hii imewafanya watu wengi wasipende kuomba kwa sababu kuomba imekuwa uzoefu wa kukatisha tamaa katika maisha yao. Unaweza kuliona hili katika maisha ya wakristo na hata makanisani, waombaji ni wachache pamoja ya kuwa wanajua kuna umuhimu wa kuomba kwa ajili yao binafsi, kazi ya Mungu na Miji/taifa.
Kumbuka biblia inasema mtu hapewi taji asiposhindani kwa uhalali. Neno “uhalali” linamaanisha kanuni au sheria za mashindano. Huwezi kutunukiwa zawadi kwasababu tu umefunga goli au umekimbia ukawatangulia wenzako wote. Pamoja na hayo ushindi wako utahalalishwa na kama ulifuata KANUNI.
Kitabu hiki kitaachilia ndani yako roho ya maombi na kukufundisha “KANUNI” ambazo kwazo maombi yako yatakuwa yenye matokea ya ushindi. Kimeambatanishwa shuhuda hai zitakazochochocea kiu yako ya kuomba kwa namna isiyokuwa ya kawaida.
Key Topics Covered:
Maana ya Maombi (Meaning of Prayer)
Kile ambacho maombi yanaweza kufanya
(What prayer can do)
Aina za maombi (Types of prayer)
Jinsi ya kuomba ili ujibiwe (How to pray to receive answers)
Shuhuda za kimaombi (Prayer testimonies)
Vikwanzo vya maombi (Obstacles to prayer)
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Godfrey Ngaleya