Your Basket

Checkout | Shopping Cart
Nilipojigeuza Mwanamke - GetValue
Biashara & Ujasilimia Mali

NILIPOJIGEUZA MWANAMKE

0
0
  • 5
  • 4
  • 3
  • 2
  • 1
Price:
1,000 Tsh.
Vendor:
Added To Cart:
0
Added to shop:
Oct 19, 2022
Product Views:
568
In category:
Sample

NILIPOJIGEUZA MWANAMKE ILI KULIPIZA KISASI KWA PROFESSOR ALIYENIFUKUZA CHUO

*SEHEMU YA 01

 

"hodi wenyewe hodiiii!" nilibisha kwenye geti la mlango wa jumba moja kubwa huku nikigonga kwa kutumia mkono geti hilo, siyo kwamba nilikuwa sijui kama kuna switch ya kengele, la hasha, ila ni kwa sababu tu nilitaka nionekane mshamba mbele ya mwenyeji wa nyumba hiyo ili lengo langu la kuingia na kuishi kama mfanyakazi wa ndani ndani ya nyumba hiyo litimie

 

"karibu, nani wewe?" sauti ya mwanamke iliniitikia baada ya kugonga geti na kuita kwa muda mrefu bila majibu na mtu huyo akafungua geti na kunitazama

 

"shikamoo!" nilimsalimia kwa kupiga goti (kuchuchumaa kidogo) mama huyo akabaki akinitazama tangu chini mpaka juu kisha akanishusha juu mpaka chini

 

"marahaba nani wewe?"

"naitwa Beata mama!" niliongea kwa kubana sauti ya kike

"shida yako mpaka unagonga gonga geti kama mwizi wakati switch ya kupigia kengele ipo?"

"sikujua mama kama kuna pa kubonyezea sijazoea mambo hayo!"

"sema shida yako nina mambo kazi nyingi za kufanya"

"nilikuwa naomba kazi!"

"kazi gani?"

"yoyote tu ile mama yangu nitaifanya kwa bidii!"

"mh wewe umesoma mpaka kidato cha ngapi mpaka uombe kazi kwenye nyumba hii una vyeti?"

"hapana nimeishia darasa la tano tu mama wazazi wangu hawakuwa na pesa za kunisomesha"

 

"ooh hapa hakuna kazi yoyote si ukatafute maofisini huko?"

"hata kazi za ndani naweza kufanya dada yangu!"

"nimekwambia hapa hakuna kazi yoyote sijui umenielewa wewe dada?"

"sawa dada asante!" nilijibu kiunyonge nikageuka na kuondoka ila kwa upelelezi nilioufanya nilishapata taarifa za kuwa nyumba hiyo ya profesa mmoja wa chuo kikuu aitwae profesa Nguza ilikuwa haina mfanyakazi wa ndani au dada wa kazi 'house girl' baada ya aliyekuwepo kufukuzwa kwa sababu ya wizi

 

 Nilipotembea hatua tano tu kwa mwendo wa kiusichana na kiunyonge

 

"wewe msichana!" yule mama aliniita tena

"abee" nilimwitikia kiunyonge na kugeuka kumtazama akaniita kwa ishara ya mkono nikageuka na kurudi kumfuata tena mpaka getini

 

"umesema unaitwa nani?"

"Beata dada"

"unatokea mkoa gani?"

"Shinyanga kijiji cha (.....)" nilimjibu akatikisa kichwa na kuniangalia kwa sekunde kadhaa kisha

 

"sawa umesema kazi za ndani unaziweza?"

"ndiyo dada"

"kupika, kufua, kupasi kuosha vyombo??"

"vyote naviweza dada!"

"una mdhamini?"

"hapana nimeingia jana kutoka Shinyanga sina ndugu yeyote hapa Dar"

"mh sasa inakuwa ngumu kukuamini?"

"niamini tu dada sina shida unaweza kunijaribu tu!" nilimjibu mkono mmoja nikiwa nimeushika mfuko wangu wa rambo wa nguo na mkono mwingine nimeshika gauni langu refu la kishamba shamba lililokuwa linaburuzika chini

 

"anyway unaweza kuingia ndani tukazungumza zaidi maana nilikuwa nahitaji dada wa kazi"

"asante dada!" nilijibu tukaingia ndani mimi na mama huyo na kumbe kulikuwa na mlinzi ambae alikuwa amelala tu kwenye chumba chake pale getini, mama huyu mwenye nyumba akamlalamikia kwa kutokunisikia wakati nagonga geti muda wote, mlinzi huyo akaomba msamaha baada ya kukurupushwa kutoka usingizini kisha akatoka na kurudi getini huku akinitazama mimi na kunikonyeza wakati nikipita

 

 Tuliingia na yule mama mke wa profesa tukafika sebuleni akanikaribisha kukaa nikakaa kwenye kochi nikishangaa shangaa nikijifanya mshamba wa vitu hivyo

 

"karibu sana Beata hapa ndiyo nyumbani kwangu naishi mimi tu na mume wangu watoto wametawanyika wapo mashuleni na vyuoni"

 

"asante dada pazuri"

"jisikie upo nyumbani utatumia kinywaji gani soda au juisi?"

"juisi tu!"

"ooh nilidhani nawewe utasema maji kama watu walivyojizoesha"

"hahaha dada!" nilicheka nae akacheka na kulifuata friji ili kunichukulia juisi nami wakati huo nikayashika matiti yangu feki niliyoyapachika kifuani na kuyaweka weka vizuri maana matambara yalianza kushuka shuka kwenye sidiria niliyoivaa

 

 Mama huyo aliniletea glasi ya juisi ambayo niliipokea na kumshukuru tena na wakati huohuo honi ya gari ikasikika nje ya geti mlinzi akafungua geti na mama huyu akatoka na kwenda kuupokea ugeni huo nami nikasimama na kuchungulia dirishani nikaona gari likipaki na akashuka baba mmoja mtu mzima nilipomtazama vizuri alikuwa ni profesa Nguza ambae ndiye niliyekuwa namtafuta haswa mzee huyu ambae hatonitoka kichwani mwangu kutokana na aliyoyatenda ambayo yameweka kumbu kumbu isiyofutika moyoni mwangu

 

 Wawili hao mtu na mkewe waliingia sebuleni na kunikuta nimekaa nikizikuna kuna nywele zangu za 'twende kilioni' na haikuwa rahisi kwa mtu kugundua kuwa mimi ni mwanamke kwa jinsi nilivyojipodoa nikapodoka ingawa kwa mbali sana ili nionekane mwanamke tu na siyo mrembo kwa sababu ninajifanya nimetokea kijijini na uzuri hata sura yangu nimeirithi kwa mama ni nzuri nzuri hivi

 

"mume wangu dada wa kazi tumempata ni huyu hapa anaitwa Beata!" mama huyo alinitambulisha

"shikamoo baba!" nikamsalimia kwa heshima

"marahaba!" mzee huyo aliniitikia juu juu tu kisha akaendelea na safari yake kuelekea chumbani akiwa ameonekana wala hajanifurahia kivile nami nikaliweka gauni langu vizuri na kukaa taratibu

 

"hatimae nimekuona adui yangu!" nilijisemea kimoyo moyo huku nikitabasamu nikiwa tayari ndani ya nyumba hiyo kwa ajili ya kazi maalum 'mission' iliyonileta ya kulipiza kisasi....

More Products On Discount
More Products From This Seller
Best Sellers List
Best Seller
2,000 Tsh.
(5.4)

Sold by: Gaston Ngailo

Best Seller
10,000 Tsh.
(69.8)

Sold by: Samuel Macha

Best Seller
3,000 Tsh.
(16.4)

Sold by: ABDULKADIR MASSA

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PETER TARIMO

Best Seller
4,000 Tsh.

Sold by: Mashaka Khamis

GetValue Recommendations
5,000 Tsh.

Sold by: Denis Mpagaze

10,000 Tsh.
(1)

Sold by: PJ PROJECTS

12,000 Tsh.

Sold by: Germano Mbelwa

5,000 Tsh.

Sold by: Sabas Patrick

25,000 Tsh.

Sold by: PJ PROJECTS

Old is Gold