Your Basket

Checkout | Shopping Cart
Nilijifanya Kipofu Ili Kuona Kama Ni Kweli Mke Wangu Anamahusiano Na Mdogo Wangu - GetValue
Biashara & Ujasilimia Mali

NILIJIFANYA KIPOFU ILI KUONA KAMA NI KWELI MKE WANGU ANAMAHUSIANO NA MDOGO WANGU

0
0
  • 5
  • 4
  • 3
  • 2
  • 1
Price:
3,000 Tsh.
Vendor:
Added To Cart:
0
Added to shop:
Oct 19, 2022
Product Views:
2,152
In category:
Sample

SIMULIZI YA KWELI....

NILIJIFANYA KIPOFU ILI KUONA  KAMA NI KWELI MKE WANGU ANAMAHUSIANO NA MDOGO WANGU


EP 01.

Mke wangu Suzy na mdogo wangu Max walipenda kuitana majina  mengi tu ya kimahaba, wakati mwingine waliitaka mbele yangu lakini sikuwafikiria vibaya hata siku moja, kuna wakati Suzzy alimuita Max. "mume wangu, honey, sweet" na majina mengine tu mazuri ambayo wapenzi huitana, kwangu mimi niliona ni kawaida kwani mimi na Max ni ndugu wa damu na wala sikuwahi kufikiria kama  Max anaweza kutembea na mke wangu Suzy.


ANZA NAYO..

Baada ya mke wangu kwenda kulala na mimi nikazima Tv kisha nikamfuata chumbani kwani siku hiyo nilikuwa nina ham naye sana. Nilipoingia chumbani nilimkuta mke wangu Kalala, kavaa bukta mbili na jinsi ngumu sana kisha akafunga na kimkanda kigumu kweli. Nilishangaa sana kwani haikuwa tabia yake "Suzzy Suzzy" Nilimuamsha kwa kumtikisa.


"Moris bwana mie nina usingizi mbona una kero hivyo wewe mwanaume!" aliniambia mke wangu huku akigeuka ukutani na kunipa mgongo. "Mh this is too much!" Nilijisemea mwenyewe huku nikivua nguo zangu na kupanda kitandani. 


Uchu ulinizidia bado niliendelea kumsumbua mke wangu. "Moris tusitiane majaribuni mimi nipo kwenye mfungo wa maombi ya siku 100, nipo kwenye maombi ya kuombea familia yetu" alisema mke mke wangu.


"Hata kama kwani mimi si mumeo wa ndoa, Kwahiyo huyo mchungaji wenu ndio anawafundisha kuwa mkiwa kwenye mfungo au maombi msiwape wanaume zenu haki za ndoa zao" Nililalamika usiku huo sana lakini mke wangu alizidi kutoa visingizio vingi.


"Sio hivyo mume wangu jali na afya ya mwenzio, mie mchana sili, nipo kwenye maombi mazito, unafikiri tukifanya hivi si unanichosha sana na kunikondesha, naomba uwe mvumilivu mume wangu, kwani siku  100 ni nyingi?" Aliniuliza mke wangu.


"Ni nyingi sana na mbaya zaidi hukunishirikisha!" Nilimwambia. "Basi poa mimi sipo tayari nimuache Mungu wangu kwasababu ya tamaa zako za kimwili, ukiamua kuchepuka ruksa! Ukiamua kuwa mvumilivu sawa lakini ni lazima nimalize mfungo wa siku 100 bila kuguswa mwili wangu!" alisema mke wangu kwa jeuri, hakuwahi kunijibu hivyo kabla, tulipendana sana tena sana, Nilijikuta machozi yakinitoka.


Nilienda kwa watu wengi wenye hekima na ambao ndoa zao zina utulivu, niliomba ushauri, kila mmoja aliniambia kuwa hata kama yupo kwenye maombi lakini kila jambo hufanyika kwa kiasi biblia yenyewe imeagiza. Wengine waliniambia labda kama ningekuwa sina ndoa naye basi ni sahihi kunifanyia hivyo, wengine walidai kuwa tayari kuanza kuchepuka ndio maana mapenzi yamepungua lakini ajabu yeye na mdogo wangu walizidi kupendana sana, kuwa na ukaribu sana uliopitiliza japo sikuwahi kuwafumania kwa jambo lolote la kimapenzi lakini roho yangu iliutilia mashaka upendo wao, niliamua nichunguze mwenyewe kwa kujifanya nimepofuka macho kusudi nione kama wana mahusiano yoyote ya kimapenzi! Siku ya kwanza kujidai nimepofuka macho hawakuamini mpaka nilipojikaza ndani ya siku nne bila kwenda kazini, chooni walinipeleka, chakula walinilisha na hapo wakaamini kweli nimepofuka macho. Jioni moja tukiwa tumekaa sebuleni ghafla nikashangaa...


JE NINI KILIENDELEA? WANGAPI MPO TAYARI KWA EPISODE INAYOFUATA...

More Products On Discount
More Products From This Seller
Best Sellers List
Best Seller
2,000 Tsh.
(5.4)

Sold by: Gaston Ngailo

Best Seller
10,000 Tsh.
(69.8)

Sold by: Samuel Macha

Best Seller
3,000 Tsh.
(16.4)

Sold by: ABDULKADIR MASSA

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PETER TARIMO

Best Seller
4,000 Tsh.

Sold by: Mashaka Khamis

GetValue Recommendations
5,000 Tsh.

Sold by: Denis Mpagaze

10,000 Tsh.
(1)

Sold by: PJ PROJECTS

12,000 Tsh.

Sold by: Germano Mbelwa

5,000 Tsh.

Sold by: Sabas Patrick

25,000 Tsh.

Sold by: PJ PROJECTS

Old is Gold