Your Basket

Checkout | Shopping Cart
Thawabu Kwa Mvunaji Nafsi - GetValue
Biashara & Ujasilimia Mali

THAWABU KWA MVUNAJI NAFSI

0.2
1
  • 5
  • 4
  • 3
  • 2
  • 1
Price:
10,000 Tsh.
Added To Cart:
0
Added to shop:
Jul 05, 2026
Product Views:
87
In category:
Sample

THAWABU KWA MVUNAJI NAFSI rnKwa nini Kila Mkristo Ameitwa Kuokoa WaliopotearnrnKitabu hiki kinafunua wito wa Mungu kwa kila Mkristo wa kushiriki katika kuwaokoa waliopotea na kueleza thawabu kuu zinazowangoja Wavunaji nafsi. Kitakuhamasisha kuishi kwa kusudi, kuhubiri Injili kwa ujasiri, namna ya kushinda vikwazo KATIKA Uinjilishaji na kukuonesh Namna utaweza WEKEZA maisha yako katika kile chenye thamani ya milele.

Katika kila kizazi, Mungu huwainua watu wakike na wakiume ambao mioyo yao huwaka kwa shauku moja ya kuona maisha yakibadilishwa kwa uweza wa Injili. Kitabu hiki, Thawabu kwa Mvunaji Nafsi: Kwa Nini Kila Mkristo Ameitwa Kuokoa Waliopotea, kimezaliwa kutokana na mzigo huo wa ndani wa ki-Ungu na wito ulio wa Upesi katika kuwaokoa waliopotea.


Maana tunaishi katika nyakati ambazo sauti za ulimwengu zazidi kuwa nyingi, bali kilio cha milele cha waliopotea hakisikiki kwa wengi. Watu wengi wanapotea kila siku bila tumaini, wala mwelekeo, wala kumjua Kristo aokoaye. Lakini mbinguni, hufurahi pale mwenye dhambi mmoja akitubu.

Kwa hiyo, jambo hili latukumbusha ya kwamba utume ulio mkuu kuliko yote duniani haujabadilika kamwe kuokoa waliopotea.

Maana kuokoa nafsi si kazi ya wachache tu, bali ni wajibu mtakatifu wa kila mwamini. Wala si huduma tu, bali ni shauku kuu ya moyo wa Mungu mwenyewe. Tangu mtu apokeapo neema ya wokovu katika Kristo Yesu, hukabidhiwa ujumbe wenye uzito wa milele (2 Wakorintho 5:17-20)

Kitabu hiki kimelenga kuamsha ufahamu na kuchochea shauku mpya kwa kila msomaji.

Ndani ya kurasa hizi, utaona si wito wa kuhubiri Injili tu, bali pia thawabu zake kuu, zipatikanazo kwa wale wajitoao kwa ajili ya waliopotea. Thawabu hizi hazingoji mbinguni pekee, bali huanza hata sasa zikidhihirika kama furaha, na kusudi, na ukuaji wa kiroho, na kushirikiana na Mungu mwenyewe. Zaidi ya Baraka zote za duniani ipo heshima kuu ya kuona maisha yanaokolewa na hatima za watu nikirejeshwa.

Kazi hii imeandikwa ili kuwahamasisha, na kuwafundisha, na kuwachochea waamini katika kila hatua ya imani yao. Ikiwa u mchanga katika imani, au u mtumishi wa muda mrefu wa kazi ya Bwana, neno ni lile lile: umeitwa, umechaguliwa, nawe umetumwa.

Basi, usomapo, moyo wako na uchochewe kwa huruma; imani yako na ithibitishwe kwa nguvu; na roho yako na iwashwe kwa ujasiri. Uanze kuwaona watu si kama walivyo sasa, bali kama watakavyokuwa katika Kristo. Na upokee Heshima ya kuwa mtendakazi pamoja na Mungu katika jukumu kuu tulilopewa wanadamu.

Mavuno yapo tayari. Wito umekwisha kutolewa. Wakati ni sasa.

Je! Uko tayari kwenda?

More Products On Discount
Best Sellers List
Best Seller
1,000 Tsh.
(5.4)

Sold by: Gaston Ngailo

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PASTOR TONY OSBORN

Best Seller
10,000 Tsh.
(69.8)

Sold by: Samuel Macha

Best Seller
3,000 Tsh.
(16.4)

Sold by: ABDULKADIR MASSA

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PETER TARIMO

Best Seller
25,000 Tsh.
(3.6)

Sold by: Gaston Ngailo

GetValue Recommendations
Old is Gold