.jpg)
Uponyaji Wa Kiungu Divine Healing
UPONYAJI WA KIUNGU(DIVINE HEALING)\r\nNdani ya kitabu hiki kilichojaa Ufunuo na siri nyingi zilizokuwa zimefichwa (Hidden Mystery) utakutana na Uponyaji wa Mungu usomapo na itakupa hasira ya kumfukuza Shetani na mapepo yake na kuongeza ujasiri wako ndani ya Kristo Yesu.Kuna ufahamu uliokuwa umefichika ndani ya Kristo na ndani ya wale wamwaminio ila kwa kusoma kitabu hiki zitakuwa wazi mbele yako(Efes.3:8-9”nalipewa neema hii ya kuwahubiri Mataifa utajiri wake Kristo usiopimika;na kuwaangaza watu wote wajue habari za madaraka ya siri hiyo, ambayo tangu zamani zote ilisitirika katika Mungu aliyeviumba vitu vyote”)\r\nMiongoni mwa maswali tata yatakayojibiwa ndani ya kitabu hiki cha Uponyaji wa Kiungu(Divine Healing) ni kama vile:-\r\n1.Nini Asili ya magonjwa na vilema?\r\n2.Anguko la Lusifa\r\n3.Lusifa(Shetani) alianguka lini na Je; alianguka mara ngapi au kutupwa mara ngapi?Kwa sababu Isay.14:12 inatuambia Shetani(Lusifa) alianguka na pia Ufun.12:14 tunaona Shetani/Ibilisi akitupwa tena.\r\n4.Je; Mapepo(devils/evil spitrits/demons) ni Malaika walioasi au Malaika walioasi(Fallen Angels) ni tofauti na mapepo\r\n5.Nadharia ya Gap Theory; Je kuna Gap kati ya Mwanz.1:1 na Mwanz.1:2;Je; Biblia inasemaje?\r\n6.Mbingu tatu(Three Heavens) na ukweli wake kutoka kwenye maandiko\r\n7.Kwanini mapepo yanaitwa Dis-embodied spirits na wao ni earthly bound wakati Malaika walioasi(waitwao Falme na Mamlaka kwenye Efes.6:12) wao ni Heavenly bound yaani wanafanya kazi kutokea mbingu ya pili\r\n8.Je; Mtu aliyeokoka anaweza kuingiwa na mapepo(yaani kuwa possessed by evil spirits) au kupagawa na nguvu za mapepo(devils)?\r\n9.Vitu gani mtu akivifanya vinaweza kufungua mlango ulio wazi kwa mtu kufungwa na vifungo vya Nguvu za giza na kufungua uhalali kwa Shetani kumfunga mtu na kumletea mateso\r\n10.Nini kinasababisha mtu aliyefubguliwa kutoka kwenye nguvu za giza na mapepo afungwe ten ana mapepo na kurudi tena ndani ya mtu\r\n11.Mapepo yakimuingia mtu yanakaa wapi? Je; yanakaa kwenye roho(spirit), Nafsi(soul) au mwili(body)?\r\n12.Dalili za mtu mwenye mapepo au aliyepagawa na mapepo\r\n13.Jinsi gani ya kuwaombea watu waliofungwa na mapepo na nguvu za giza.\r\n14.Jinsi ya kupata ushindi dhidi ya mapepo na Nguvu za Giza kupitia kutambua na kufahamu Mamlaka(Exousia) na nguvu(Dunamis) iliyopo ndani ya muamini.\r\n\r\nNi maombi yangu Mungu akupe Neema kujifunza na kuyaelewa usomapo haya ili kuweza kutembea na kuishi kwa ushindi katika Maisha yako ya kila siku.Kwani tumekusudiwa tuishi Maisha ya ushindi ndani ya Kristo Yesu aliye Bwana na mwokozi wetu.\r\n\r\nKaribu sana tujifunze.
Kitabu cha Upinyaji wa kiungu(Divine Healing) kinaweka wazi siri zihusuzo Mungu mponyaji.Katika dunia iliyojaa magonjwa yasiyotibika na hofu za kila Namna ninaamini kuna tumaini ndani ya Mungu aliye chanzo cha uzima na Uponyaji.Ni kweli taalama za kitabibu zipo na kutokana na ukuaji wa Sayansi na Teknolojia kuna mavumbuzi mengi ila bado tumaini lipo kwa Mungu maana kuna mengine akili za mwanadamu zina ukomo.