HATUA 6 ZA KUJIAJIRI
Kama umeajiriwa lakini una shauku ya kuacha ajira na kuanza kufanya mambo yako, andiko hili ni zawadi kwako. Nimeweka hatua zilizotumia kuacha ajira na kufanikiwa kujiajiri.
Mwaka 2016 mwezi wa 8 niliweza kuacha ajira na kujiajiri. Kazi niliyokuwa nafanya ya ualimu kwa kipindi hicho cha miaka 8. Ni nadra sana mwalimu kuacha ajira kwa sababu kwa kipindi hicho, hakuna shule inayoajiri. Lakini pia ni kipindi ambacho waajiri wengi wanapitia kipindi kigumu. Mishahara inachelewa kutoka.
Nakuandikia haya sio kwamba nimesoma vitabu vingi kuhusu mada hii; hapana!! Nakuandikia haya majibu kwa sababu nilipitia huo mchakato wa kutoka kwenye ajira kwa hiara nikilenga kufanya kazi niliyotamani kwa miaka mingi; kazi ya kuelimisha jamii na kuandika vitabu. Ninapoandika maneno haya, nina miaka mitatu tangu niachane na utaratibu wa mshahara.
Nimejifunza mengi na nimekutana na wengi wanaopambana na hali ya kuacha ajiri ili wafuate ndoto zao. Kama wewe ni muajiriwa mwenye kiu ya kujiajiri kwa nia ya kufuata ndoto yake, basi utapata majibu humu.Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza